Trump alikosoa mara chungu nzima makubaliano hayo ya nyuklia na kuyataja kuwa, makubaliano mapya kabisa kwa Marekani na akatishia kuitoa nchi yake. Baada ya Marekani kujitoa katika makubaliano ya nyuklia, serikali ya Trump iliacha kutekeleza ahadi ilizotoa kwa mujibu wa makubaliano hayo na kwa mujibu wa azimio nambari 2231 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Marekani ilichukua hatua hiyo licha ya upinzani mkubwa duniani na ikiwa na lengo la kuilazimisha Iran ikibaliane na matakwa yake haramu ilianza kutekeleza vikwazo ambavyo havijawahi kushuhudiwa katika fremu ya wenzo wa mashinikizo ya kiwango cha juu kabisa dhidi ya Tehran. Si hayo tu, bali Marekani ikawa ikipinga kila mpango wowote wenye lengo la kuyalinda na kuyabakisha makubaliano hayo ya kimataifa.
Kujitoa Marekani katika makubaliano ya JCPOA haukuwa uamuzi binafsi wa Donald Trump bali ilikuwa hatua iliyotokana na sehemu kubwa ya mamlaka ya kisiasa ya Marekani hususan chama cha Republican ambacho kimsingi kilikuwa kikipinga makubaliano hayo. Hatua ya Marekani ilikuwa kinyume kabisa na vipengee vya makubaliano ya nyuklia pamoja na azimio nambari 2231 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Kimsingi hatua hiyo ilikuwa ni ya kimabavu na ililenga kuyazuia mataifa mengine kuwa na ushirikiano wa teknolojia ya nyuklia na Iran.
Ukweli wa mambo ni kuwa, katika kipindi cha uongozi wa Donald Trump, kwa hatua yake ya upande mmoja ya kujitoa katika JCPOA, Marekani ilifanya ugaidi wa kiuchumi kwa kutumia wenzo wa mashinikizo ya kiwango cha juu kabisa dhidi ya Iran. Kujiondoa Marekani katika makubaliano hayo, kuliambatana na mashinikizo makubwa ya kiuchumi dhidi ya Iran hali ambayo iliwafanya wananchi wa Iran kuzidi kukabiliwa na matatizo ya kimaisha.
Siyo tu kwamba, hatua ya Marekani ya kujiondoa katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA haijaweza kuzuia Iran kusonga mbele mpango wa nyuklia wa Iran, bali nafasi ya kijeshi, kiulinzi na kieneo ya Iran imeimarika zaidi. Mkabala na “mashinikizo ya kiwango cha juu kabisa” Iran ilitoa jibu la hilo kwa sera ya “kusimama kidete kwa kiwango cha juu kabisa”. Mbali na hayo kujitoa Marekani katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA kulifunga milango ya ushirikiano baina ya Iran na madola ya Magharibi na badala yake hilo likawa na maslahi kwa ajili ya kupanuliwa ushirikiano baina ya taifa hili na mataifa ya Russia na China.
Serikali ya Trump ilikuwa ikidai kwamba, kwa kuanzisha wenzo wa mashinikizo ya kiwango cha juu kabisa itaweza kuilazimisha Iran isalimu amri mbele ya matakwa yake 12 ambayo yalitangazwa Mei 2018 na Mike Pompeo aliyekuwa Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani wakati huo.
Pompeo alitoa orodha ya mambo 12 kama masharti yanayopaswa kutekelezwa kala ya Washington kufanya mazungumzo na Tehran ambayo yalifanyiwa dhihaka na akthari ya wachambuzi wa mambo na vyombo vya habari. Miongoni mwea masharti hayo ni kusimamishwa kikamilifu mpango wa nyuklia wa Iran, kusimajmishwa mpango wa makombora wa Iran na kuhitimishwa hatua za Iran katika eneo la Asia Magharibi. Matakwa ya Pompeo yalikuwa na maana ya Iran kujisalimisha kikamilifu kwa marekani. Mtazamo wa serikali ya Trump ulikuwa kwamba, mashinikizo ya kiwango cha juu kabisa yanaweza kuifanya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilazimike kukaa katika meza moja ya mazungumzo na Marekani kwa ajili ya makubaliano mpaya badala ya JCPOA.
Hata hivyo Januari 2021, Trump aliondoka madarakani baada ya kushindwa katika uchaguzi wa Rais huku mipango yake dhidi ya Iran ikiwa imefeli na kugonga mwamba. Hata mtu mwenye misimamo mikali kabisa katika serikali ya Tump yaani John Bolton aliyekuwa mshauri wa usalama wa taifa amekiri hizo wazi na pasi na kificho.
Kusimama kidete kwa kupigiwa mfano kwa wananchi wa Iran mkabala wa vikwazo hivi katika kivuli cha sera za kusimama kidete kwa kiwango cha juu kabisa ni jambo ambalo liliikatisha tamaa serikali ya Trump na kuifanya ishindwe kufikia malengo yake haramu. Hili ni jambalo ambalo wamekiri akthari ya wajuzi wa mambo na viongozi wa kisiasa wa ndani na nje ya Marekani. Miongoni mwao ni Antony Blinken, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani ambaye amesema kuwa, hatua ya Trump ya kuiondoa Marekani katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA ulikuwa uamuzi mbaya kabisa katika historia ya hivi karibuni katika sera za kigeni za Marekani.
Chris Murphy, seneta wa chama cha Democratic ameandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter kwamba: Tukumbuke kwamba, Marekani haijapata kitu chochote kupitia vikwazo vya Trump…vikwazo hivyo havijawa na taathira yoyote ya kivitendo.”
Wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka 2020, Joe Biden alikiri kwamba, Trump alifanya kosa kujitoa katika makuba;liano ya nyuklia ya JCPOA, alichukua hatua zinazokinzana na maslahi ya Marekani na akaifanya Washington itengwe. Pamoja na hayo, tangu Biden aingie madarakani amefuata mkondo wa mashinikizo ya kiwango cha juu kabisa dhidi ya Iran.
Nukta muhimu ni hii kwamba, licha ya kuwa Marekani imejiondoa katika makuabliano ya nyuklia ya JCPOA, lakini wakati huo huo haitaki kuona kukitangazwa kifo cha makubaliano hayo na kuingia katika ulimwengu ambao hauna makubaliano hayo.
342/