Al-Miqdad amebainisha kuwa, kurejeshwa katika hali ya kawaida uhusiano wa Syria na Uturuki hakutafanyika ila tu baada ya kuondolewa vikosi vya nchi hiyo katika ardhi ya Syria.Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria ameongeza kuwa hata mkutano kati ya Rais Bashar Assad wa Syria na mwenzake wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan unategemea kuondoka vikosi vya jeshi la Uturuki nchini Syria.Aidha, Al-Miqdad ameashiria ushindi mkubwa liliopata jeshi la Russia nchini Ukraine na kuongeza kuwa: Marekani na nchi za Magharibi zilishadidisha hatua za kichochezi na mara nyingi kutoa kauli za uwongo, na kwamba jambo hilo ndilo lililosababisha Moscow kuchukua hatua ya kijeshi ambayo Damascus inaiunga mkono.
Kuhusiana na mkutano wa hivi karibuni wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria amesema: "tulishuhudia moyo wa upendo wakati wa mkutano wa viongozi wa Kiarabu huko Jeddah ulioonyeshwa kwa watu na viongozi wa Syria, na tunahisi kwamba viongozi na wananchi wa mataifa ya Kiarabu daima wamekuwa na mapenzi na sisi, kwa sababu Syria iko mstari wa mbele katika kushikamana na malengo ya Umma wa Kiarabu.
Al-Miqdad, vilevile amelaani kitendo cha Israel cha kuendelea kuishambulia kijeshi Syria na kuionya Tel Aviv kwa kuitaka ikomeshe hatua na vitendo vyake vya jinai na uchokozi.Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria amesisitiza pia kuwa, Damascus inazitegemea nchi za Kiarabu kuwa zitasimama upande wa Syria katika kukabiliana na uchokozi wa Israel.../
342/