Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran leo Jumanne anaanza safari ya kuzitembelea nchi hizo tatu kwa ajili ya kuimarisha ushirikiano na nchi za bara la Afrika. Safari hiyo inakuja kufuatia mwaliko rasmi wa marais wa Kenya, Uganda na Zimbabwe.
Nasser Kanani, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran alisema hayo katika mkutano na waandishi wa habari siku ya Jumatatu, akijibu swali la mwandishi wa habari wa Iran Press na kuongeza kwamba ziara ya Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, barani Afrika ni fursa nzuri kwa hatua mpya katika mchakato wa ushirikiano wa pamoja kati ya Iran na nchi hizo tatu.
Aidha ameeleza kuwa, bara la Afrika lina uwezo mkubwa wa kiuchumi na kuongeza kuwa: "Uchumi wa Afrika ukiwa katika mzingo wa ukuaji sasa unazingatiwa na nchi nyingi muhimu duniani"
Kanaani amesema: "Kutokana na kuwepo kiwango kikubwa cha maliasili barani Afrika, Iran inaweza kutoa msaada mkubwa kwa bara hili kutokana uwezo wake katika nyanja ya teknolojia na maarifa.
Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amesema: "Nchi za Kiafrika zina nia ya kupanua uhusiano na Iran na safari hii italeta ushirikiano wa kisiasa na kiuchumi baia ya pande mbili."
342/