Dmitry Peskov, msemaji wa Kremlin, amesema kwamba mashambulizi ya Ukraine yaliyolenga maeneo tofauti ya Russia hayakufanikiwa kama ilivyokuwa imepangwa, na rasilimali za NATO zilipotea bure.
Peskov ameongeza kuwa: Mashambulizi ya Ukraine hayakufua dafu kama ilivyopangwa, na rasilimali za mabilioni ya dola za NATO zinatumiwa bila ufanisi na bila malengo.
Msemaji wa Ikulu ya Rais wa Russia, Kremlin amesema: Sera ya Marekani kuhusu Ukraine inakinzana na viwango vya kimataifa na itapelekea kuvurugika usalama zaidi barani Ulaya.
Kuhusu shambulio la ndege zisizo na rubani za Kiev kwenye eneo la biashara mjini Moscow, afisa huyo wa ngazi za juu wa Russia amewaambia waandishi wa habari kwamba: Russia itachukua hatua zaidi kujilinda dhidi ya mashambulizi ya ndege zisizo na rubani za Ukraine.
Ndege mbili zisizo na rubani za Ukraine zilizokuwa zikipanga mashambulizi mjini Moscow zilidunguliwa magharibi mwa jiji hilo mwendo wa saa 3:45 asubuhi Jumapili (Julai 30).
Inasemekana kwamba hakukuwa na majeruhi katika tukio hili, na kwamba limesababisha uharibifu mdogo kwenye majengo mawili ya ofisi mjini Moscow.
342/