Wizara
ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hivi karibuni
ilitoa taarifa inayoeleza kuhusiana na kuachiliwa rasilimali za Iran
zinazoshikiliwa nje ya nchi, na vilevile kuachiwa huru idadi kadhaa ya
wafungwa waliokuwa wakizuiliwa kinyume cha sheria nchini Marekani.
Taarifa ya Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilisema: Mchakato wa kuachiliwa mabilioni kadhaa ya dola, mali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, yanayoshikiliwa kinyume cha sheria na Marekani kwa miaka kadhaa nchini Korea Kusini umeanza, na Iran imepata dhamana inayohitajika kwamba Marekani itatekeleza wajibu wake katika suala hili.Akizungunmza jana katika kikao na baraza lake la mawaziri, Seyyid Ibrahim Raisi, alisema: Kuachiliwa sehemu ya rasilimali za fedha za kigeni za nchi hii ni hatua yenye thamani, fahari na inayoendana na maslahi ya taifa.
Mazungumzo kati ya Iran na Marekani kuhusu mabadilishano ya wafungwa wa pande mbili na kuachiliwa fedha za Iran zilizozuiwa nje ya nchi yamekuwa yakiendelea kwa muda mrefu, kwa njia zisizo za moja kwa moja na za moja kwa moja pia. Mnamo Machi 2023, makubaliano ya jumla yalifikiwa kuhusu suala hili, lakini yakasimamishwa kutokana na vizingiti na masharti mapya ya Marekani.
342/