Msemaji wa HAMAS, Abdul Latif al-Qanou amepongeza operesheni
dhidi ya Wazayuni katika mji wa kaskazini wa Huwara, katika eneo la
Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na kueleza kuwa, operesheni hizo
zinatokana na ahadi ya kundi hilo la muqawama ya kuuhami Msikiti
Mtakatifu wa al-Aqsa, mkabala wa njama za Wazayuni za kuuyahudisha.
"Operesheni za silaha zitaendelea na hata kupanuliwa zaidi ili kutoa pigo kwa vikosi vya Israel na walowezi wa Kizayuni, na kuzima mpango wa serikali ya kifashisti wa eti kuunda hekalu juu ya mabaki ya Masjidul Aqsa," ameongeza al-Qanou.
Maafisa wa Israel wenye misimamo mikali na walowezi wa Kiyahudi mara kwa mara huvamia Msikiti wa al-Aqsa, kitendo cha uchochezi kinachowakasirisha Wapalestina.