Katika taarifa iliyotolewa jana Jumamosi, Ismail Haniya
ameulekezea kidole cha lawama utawala wa Tel Aviv na taasisi zake za
kijasusi kwa ongezeko la mauaji miongoni mwa Waarabu katika ardhi
zilizoghusubiwa.
Haniya amesema bayana kuwa, "Tunaubebesha dhima utawala ghasibu wa Kizayuni kwa umwagaji damu na mauaji yaliyoshtadi ndani ya ardhi (zinazokaliwa kwa mabavu) tokea 1948."
Kiongozi huyo wa muqawama amesisitiza kuwa, taifa la Palestina halina njia nyingine ya kujikomboa na kuwatimua wavamizi isipokuwa kuendeleza muqawama, uthabiti, mapigano na kuwa na umoja.
Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya HAMAS amebainisha kuwa: Vyombo vya usalama vya adui Mzayuni vimechukua hatua hatari inayolenga kuwashughulisha watu wetu katika mambo mengine, ili wasahau uhusiano wao wa kidini na kihistoria na Wapalestina wa Gaza, Ukingo wa Magharibi na walioko uhamishoni.
342/