Sambamba
na kumbukumbu ya Arubaini ya Imam Hussein (as), kumefanyika hafla ya
maombolezo kwa kuhudhuriwa na idadi kubwa ya kamati na vikundi vya
maombolezo vya wanachuo asubuhi ya leo (Jumatano) mbele ya Ayatullah
Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Akihutubia katika mkusanyiko huo, Ayatullah Khamenei, amesema, kila kikao cha maombolezo ya Imam Hussein na kutawasali kwake kunaandaa mazingira ya kuungana na nuru ya kimaanawi na mwenge wenye kuwaka Kihussein na akasisitiza kwamba: Maudhui muhimu kabisa ni kudumisha uhusiano huu na na kuyaunganisha na njia nyoofu ambapo hilo linahitajia irada na kusimama kidete
Ayatullah Khamenei amebainisha akizihutubu kamati na vikundi hivyo vya maombolezo vya wanachuo kwamba, kama mtasimama kidete mtafanikkiwa kufika kileleni na hivyo kufikia katika kielele cha utawala dini ya Mwenyezi Mungu, haki na uadilifu.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu sambamba na kusisitiza kuwa, vijana ni chimbuko la matumaini, ameashiria mahudhurio ya hamasa hususan vijana katika matembezi ya Arubaini ya Imam Hussein (as) kutoka Najaf hadi Karbala huko Iraq na pia katika miji mingine ya nchi na akawaambia vijana: “Kama ambavyo mlivyotembea kwa uthabiti kwenye matembezi ya Arubaini, basi katika njia ya utawala wa tauhidi pia mnapaswa kuwa imara, thabiti na kutotetereka huku mkiwa na irada na daima muishi maisha kama aliyoishi Imam Hussein na mbakie katika njia ya Imam Hussein (as).
342/