7 Septemba 2023 - 15:11
 Rais Raisi: Ustadi wa taifa adhimu la Iran ni kuvigeuza vikwazo na vitisho kuwa fursa

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa: ustadi wa taifa adhimu la Iran ni kuvigeuza vikwazo na vitisho kuwa fursa.

Seyyed Ebrahim Raisi, alieleza hayo jana mbele ya hadhara kubwa ya wananchi wa mji wa Darmiyan, mkoani Khorasan Kusini na kuongezea kwa kusema: "inatupasa sote tuchape kazi kwa matumaini na kufanya juhudi maradufu ili kazi na huduma zilizofanywa zikaribie zaidi kwenye ukamilikaji".   Sambamba na Arubaini ya Imam Hussein AS na katika ziara yake ya kutembelea mkoa wa Khorasan Kusini,  Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, umoja na mshikamano wa jamii, dini na lugha tofauti uliounganishwa na jina la Imam Hussein AS ni dhihirisho la kupatikana umoja wa Kiislamu, tumaini la kukaribia zama za kudhihiri Imam wa Zama AS na kujengeka ustaarabu unaotegemea dini na maadili ya kidini; na akaongeza kuwa: "Arubaini ni chimbuko, utambulisho, ghaya na lengo letu kuu, na ina mchango athirifu katika kujengeka kwa jamii na ustaarabu wa Kiislamu". 

Aidha, Rais Raisi amesema: suala linalowaunganisha watu wote wa Iran, wakiwemo Suni na Shia, ni kuwapenda Ahlul-Bayt (AS) ambao walifundisha namna ya kuishi na kufa.

  Seyyed Ebrahim Raisi ameashiria kuwa leo tunashuhudia kufanyika kwa mjumuiko mkubwa zaidi wa wanadamu na wa aina yake huko Karbala, na akaongeza kuwa: mikusanyiko ya watu katika Arubaini ni utoaji tena wa ahadi ya utiifu na baia' kwa dini, thamani za dini na Imam Hussein (AS); na kutoa ahadi tena kwa lengo tukufu la kupambana na dhulma na uonevu na kupigania haki na uadilifu duniani    Rais Raisi amekumbusha pia kuwa maadui wanataka kuanzisha uchokozi dhidi ya taifa na ardhi ya Iran ya Kiislamu, lakini kinachowazuia kufanya hivyo ni nguvu zinazotokana na damu ya mashahidi na wananchi walio macho wa Iran.../

  342/