Kauli hiyo ya Mufti wa Oman imepongezwa na kusifiwa sana kwenye mitandao ya kijamii.
Al-Khalili alisema jana Jumatano katika ujumbe wake kwenye jukwaa la "X" (zamani Twitter), kwamba "Kinachowapata ndugu zetu wa Gaza hii leo kutokana na uhalifu wa Wazayuni wanaoungwa mkono na nchi dhalimu ni sawa na kile kilichotokea katika Vita vya Ahzab. Hali ya wanafiki wa leo ni sawa na ile ya wanafiki wa jana; safu za (waumini na wanafiki) zilitengana katika kipindi hicho kigumu, kama safu hizo mbili zilivyotenga hii leo."
Mufti wa Oman amesisitiza katika ujumbe huo kwamba: "Hata hivyo, kadiri maadui wanavyoshambulia, ndivyo muumini wa kweli anavyokuwa na uhakika wa kupata nusra ya Mwenyezi Mungu.”
Sheikh Ahmed Al-Khalili ameongeza kuwa: “Tunapaswa kuzidisha imani na kujisalimisha kwa ahadi ya Mwenyezi Mungu, kwani tunaishi katika mwezi wa ushindi... Muumini anapaswa kufanya kila awezalo kuwasaidia ndugu zake wa Gaza na Palestina ili apate heshima ya dunia na Akhera. Ewe Mola tujaalie ushindi, Ramadhani ni mwezi wa ushindi."
Vita vya Al-Ahzab au Khandak, vilitokea katika mwezi wa Shawwal mwaka wa tano wa Hijra ya Mtume, baina ya Waislamu wakiongozwa na Mtume Muhammad (SAW), na makundi ya makabila tofauti ya Waarabu wakishirikiana na Wayahudi, yaliyokusanyika kwa ajili ya kuivamia Madina na kuwaangamiza Waislamu, baada ya Mayahudi wa Banu Nadhir kuvunja mapatano yao na Mtume na wakajaribu kumuua mtukufu huyo.
342/