30 Mei 2024 - 16:57
Mauaji ya Rafah katika 'Eneo Salama' yafichua ukatili wa Israeli na ushirikiano wa Washington katika mauaji hayo

Mauaji ya hivi karibuni ya raia wa Palestina katika eneo linalodaiwa kuwa "salama" katika Ukanda wa Gaza yanafichua zaidi "ukatili wa mauaji ya kimbari yanayofanywa na utawala wa Israel na ushiriki wa serikali ya Marekani katika mauaji hayo ya kimbari yanaendelea huko katika mji wa Rafah kusini mwa ukanda huo.

Haya ni kwa mujibu wa Baraza la Mahusiano ya Kiislam na Marekani (CAIR), shirika kubwa zaidi la kutetea haki za Waislamu wa Marekani.

Siku ya Jumanne Wapalestina 21 waliuawa kinyama, 12 kati yao wakiwa ni wanawake, katika mashambulizi mapya ya kikatili ya Israel dhidi ya mahema ya watu waliokimbia makazi yao, katika eneo lililotengwa na kutajwa kuwa salama huko Mawasi magharibi mwa Rafah.Katika taarifa yake siku Jumanne, Mkurugenzi Mtendaji wa Kitaifa wa CAIR Nihad Awadh alisema: "Siku baada ya siku, mauaji baada ya mauaji na utawala wa Rais Joe Biden wa Marekani unaendelea kuipa mabomu serikali ya mrengo wa kulia ya Israeli ambayo yanatumika katika kuchinja na kuwaua kinyama watoto wa Kipalestina, wanawake, wazee, wafanyakazi wanaotoa huduma za matibabu, waandishi wa habari wafanyakazi wa misaada ya kimataifa na wagonjwa waliojeruhiwa katika mashambulizi hayo ya kikatili na Marekani inaendelea kuikingia kifua Israeli dhidi ya uwajibikaji wa kimataifa. Ukatili huo wa mauaji ya halaiki ambao unafichuliwa kila siku na mirundiko ya raia wa Palestina waliochomwa moto na waliokatwa miili ipande vipande lazima ukomeshwe mara moja." Licha ya ukatili na jinai hiyo ya wazi ya Israel dhidi ya watu wa Gaza lakini kulu ya White House ya Marekani imesema hakuna mauaji ya umati wala ukiukaji wowote wa haki za binadamu unaofanywa na utawala wa kibaguzi wa Israel dhidi ya watu wa Gaza na hasa katika matukio machungu na ya kusikitisha ya hivi karibuni ya utawala huo katika mji wa Rafah kusini mwa Ukanda wa Gaza. Siku ya Ijumaa CAIR ilipongeza uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki ya Umoja wa Mataifa (ICJ) yenye makao makuu yake huko mjini Hague ya kuuamuru utawala haramu wa Israel usitishe mashambulizi yake huko katika mji wa Rafah lakini umekataa kutii amri hiyo.

342/