«.وَمَآ أَصَٰبَكُم مِّن مُّصِيبَةࣲ فَبِمَا كَسَبَتۡ أَيۡدِيكُمۡ وَيَعۡفُواْ عَن كَثِير»
"Na misiba inayo kusibuni ni kwa sababu ya vitendo vya mikono yenu. Naye anasamehe mengi."
* Wengine wanaweza kusema kwamba: Ee Mwenyezi Mungu! Kwa nini tuwe na matatizo? Aya hii inajibu swali hili kama ifuatavyo:
“Shida hizi zote zinatokana na matendo yako mwenyewe, na bila shaka, Mwenyezi Mungu amekusamehe dhambi na makosa yako mengi, vinginevyo ungekabiliwa na matatizo zaidi.”
chanzo: alanwaralmunirah