26 Novemba 2024 - 19:17
Katika Siku ya Kimataifa ya Kupinga Unyanyasaji dhidi ya Wanawake: Maandamano ya Wanawake wa Morocco kuunga mkono Wanawake wa Gaza na Lebanon

Sambamba na uadhimishaji wa Siku ya Kimataifa ya Kupambana na Ukatili Dhidi ya Wanawake, Wanawake wa Morocco walifanya Maandamano kuonyesha kuwaunga mkono Wanawake wa Palestina na Lebanon na kutaka uungwaji mkono kwa Wanawake hao (wa Palestina na Lebanon).

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul_Bayt (a.s) - ABNA - Jumatatu jioni (tarehe 25 Novemba), mamia ya Wanawake wa Morocco waliandaa maandamano katika miji kadhaa kwa ajili ya kuonyesha mshikamano wao kwa Wanawake wa Palestina na Lebanon, huku wakitaka kusitishwa kwa mauaji ya kimbari ya Israel katika Ukanda wa Gaza.

Maandamano haya yalifanyika sambamba na Siku ya Kimataifa ya Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake, inayosadifiana na Novemba 25, katika miji kadhaa kama vile Casablanca, Rabat na Tanga.

Maandamano haya yalifanyika kwa kuitikia mwito wa Safu ya Mapambano ya Morocco ili kuunga mkono Palestina na Washiriki waliinua bendera za Palestina zikiambatana na picha za Msikiti wa Al-Aqsa.