13 Machi 2025 - 17:28
Source: Parstoday
Iran ni kati ya nchi tatu zinazoongoza duniani katika kupandikiza uboho

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni miongoni mwa nchi tatu zinazoongoza duniani kwa upandikizaji wa uboho kutokana na maendeleo makubwa katika nyanja za matibabu.

Ripoti zinasema, katika miaka ya hivi karibuni, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeweza kupata maendeleo makubwa katika nyanja mbalimbali za matibabu kwa kutegemea nguvu za wataalamu wa ndani. Moja ya maeneo haya ni upandikizaji wa uboho.

Upandikizaji wa uboho umefanywa hapa nchini kwa watu walio na magonjwa kama vile leukemia au ugonjwa wa myelodysplastic, na magonjwa mengine mabaya ya damu kama vile lymphoma, myeloma na anemia ya aplastiki.

Upandikizaji huo unaweza pia kutumika katika kutibu saratani za oncological ambazo hazikubali tiba ya chemotherapy, na katika kutibu matatizo ya kuzaliwa kama vile thalassemia, ugonjwa wa seli mundu, porphyrias na matatizo makubwa ya upungufu wa kinga.

Madaktari bingwa wa Iran wameweza kuwa na jipya na kuionyesha dunia katika uga wa upandikizaji wa uboho na wamekuwa miongoni mwa nchi tatu bora duniani katika uwanja huu, kwa kadiri kwamba hivi karibuni kampuni ya Iran ilitengeneza dawa ya tiba ya seli ya allogeneic "Destrocel" mahsusi kwa wagonjwa wa upandikizaji wa uboho, ambayo ni msaada mkubwa kwa wagonjwa katika uwanja huu.

Dawa ya Destrocel inaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa matatizo ya GVHD. GVHD ni ugonjwa wa upandikizaji wa uboho ambao una hatari nyingi kwa mgonjwa.

Kuhusiana na suala hilo, Mostafa Ghanei, Katibu wa Tume ya Teknolojia ya Baiolojia, Afya na Teknolojia ya Tiba ya Ofisi ya Rais Iran alisema tarehe 29 Oktoba 2024 katika hafla ya kuzindua dawa ya Destrocel kwamba: "Iran ni moja kati ya nchi zinazoongoza katika kanda ya Asia Magharibi katika upandikizaji wa uboho, kiasi kwamba takwimu za upandikizaji uboho nchini ziko mbele sana ikilinganishwa na nchi zingine katika kanda hiyo."

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha