13 Machi 2025 - 17:29
Source: Parstoday
Yedioth Ahronoth: Kipindi cha fungate ya Trump na Netanyahu kimekwisha

Gazeti la Kizayuni la Yedioth Ahronoth limeandika katika makala kwamba baraza la mawaziri la utawala huo linaloongozwa na Netanyahu limekuwa chini kabisa ya ajenda ya Marekani.

Gazeti la Rai El-Youm limenukuu taarifa ya gazeti hilo la Kizayuni ikisema kuwa, rais wa Marekani Donald Trump hivi sasa anachukua maamuzi bila ya kumshirikisha waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu ambaye yuko chini ya amri za Washington.

Makala hiyo katika gazeti la Kizayuni la Yedioth Ahronoth inasema: "Fungate ya Trump na Netanyahu imekwisha," ikiashiria siku chache za kwanza za kuingia madarakani Trump katika Ikulu ya White House.

Gazeti hilo limeonya kuwa, ikiwa Netanyahu atakiuka maagizo ya Trump, atakabiliwa na hatima sawa na ya rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy katika Ikulu ya White House.

Gazeti hilo limebainisha kuwa, hivi sasa Marekani inawalazimisha maafisa wa Israel kutekeleza makubaliano ya mpaka wa baharini na Lebanon, ambayo huko nyuma Netanyahu aliyataja kuwa ni makubaliano ya usaliti na kusalimu amri.

Gazeti hilo limesema, wakati waziri mkuu wa zamani wa Israel Yair Lapid alitia saini makubaliano hayo na Hizbullah ya Lebanon na sasa Netanyahu analazimika kutekeleza makubaliano hayo, licha ya ahadi yake ya kuyafuta.

Yedioth Ahronoth pia limeandika kwamba, Israel imelazimishwa pia kufanya mazungumzo ya moja kwa moja na Hamas na kufikia makubaliano.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha