16 Machi 2025 - 15:40
Araqchi: Amerika haina haki ya kulazimisha (na kuelekeza) sera ya kigeni ya Iran

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa, Washington haina haki ya kulazimisha siasa za nje za Iran, na kuitaka kusimamisha mara moja mauaji yake kwa watu wa Yemen.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (AS) - Abna - Syed Abbas Araghchi, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran jana Jumapili aliandika kwenye mtandao wa kijamii wa X: Serikali ya Marekani haina haki ya kulazimisha (kuelekeza) sera za kigeni za Iran. Wakati huo uliisha mnamo mwaka 1978. 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran alisema: Mwaka jana, Biden alilaghaiwa kulipa kiasi ambacho hakijawahi kushuhudiwa cha dola bilioni 23 kwa utawala wa mauaji ya halaiki. Zaidi ya Wapalestina 60,000 waliuawa na dunia inaهwajibisha Marekani kikamilifu.

Mwishoni, Araghchi aliihutubia mamlaka ya Marekani na kuandika: Acha kuunga mkono mauaji ya kimbari na ugaidi wa Israel. Acha kuua watu wa Yemen.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha