20 Machi 2025 - 17:29
Source: Parstoday
Mdororo wa uchumi Ujerumani; Siemens kuwafuta kazi watu 6,000

Kampuni kubwa ya masuala ya uhandisi na teknolojia ya Siemens imesema inapania kupunguza kazi karibu 6,000 duniani kote, zikiwemo 2,850 nchini Ujerumani.

Afisa Mkuu Mtendaji wa Siemens, Roland Busch awali alikuwa ametangaza kupunguzwa kwa wafanyakazi kadhaa katika safu ya chini hadi wastani katika msimu wa vuli, lakini sasa ametangaza takwimu halisi za kuogofya.

Ameeleza kuwa, akthari ya wafanyakazi wa shirika hilo la teknolojia watafutwa kazi kufikia Septemba mwaka 2027. Kampuni hiyo imekuwa ikikabiliwa na mtikisiko kutokana na kupungua kwa mahitaji ya bidhaa na huduma zake.

Miungano ya kutetea haki za wafanyakazi katika nchi hiyo ya Ulaya imekosoa vikali uamuzi huo wa kupigwa kalamu nyekundu maelfu ya wafanyakazi wa Siemens.

"Hatuelewi hatua zilizopangwa na tunashangazwa na kukerwa na idadi kubwa ya ufutaji wa nafasi nyingi za ajira uliopangwa," amesema Birgit Steinborn, Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Kazi na Naibu Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi.

Naye Naibu Mwenyekiti wa chama cha IG Metall, Jürgen Kerner, ambaye pia anahdumu katika Bodi ya Usimamizi ya Siemens, pia amekosoa mipango hiyo. Amesema, "Mabadiliko hayapatikani kwa kupunguza watu, lakini kupitia mabadiliko chanya - kwa maneno mengine, kimsingi, maendeleo zaidi na mafunzo." 

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha