Kulingana na Shirika la Habari la Kimataifa la Ahl al-Bayt (a.s) - ABNA - Mamlaka ya Uturuki imetangaza kukamatwa kwa Akram Imam-oglu, Meya wa Istanbul, kama sehemu ya uchunguzi mpana wa "uanachama wake katika mashirika ya kigaidi" na "kuhusika (kujihusisha) katika ufisadi uliopangwa (na kuratibiwa)".
Kulingana na ripoti za vyombo vya habari vya Uturuki, Akram Imam-oglu alikamatwa alfajiri mnamo Machi 19, na baada ya muda wa siku nne wa kuwa katika kizuizini cha kisheria, amepangwa kufikishwa mbele ya hakimu takriban Machi 23.
Hivi sasa, kuna hali (ihtimali) nne zinazowezekana kwa maisha yake ya baadaye (kwa mustakbali wake):
1- Kuachiliwa bila masharti: Katika hali hii, Imam-oglu anaweza kuendelea kutekeleza majukumu yake kama kawaida.
2- Kuachiliwa huru sambamba na kuuzuliwa: Wizara ya Mambo ya Ndani ya Uturuki inaweza kuamua kumfukuza kazi (kumuuzulu) kwa kisingizio cha kuendelea na uchunguzi na kumteua msimamizi (mpya) wa Manispaa ya Istanbul.
3- Kuendelea kukamatwa kwa kuunga mkono ugaidi: Iwapo atashutumiwa (atatiwa hatiani) kusaidia shirika la kigaidi, anaweza kwenda jela na kuteuliwa kwa msimamizi mpya wa Manispaa ya Istanbul.
4-Kuendelea kukamatwa kwa madai ya uhalifu (ufisadi) uliopangwa na kuratibiwa: Katika hali hii, Halmashauri ya Jiji la Istanbul inaweza kuchagua rais (meya) mpya kutoka ndani ya wanachama wake, kama ilivyofanywa katika kesi (hali) za hapo awali zinazofanana na kesi (hali) yake.
Your Comment