22 Machi 2025 - 21:25
Source: Parstoday
'Uwanja wa ndege wa Ben Gurion hautakuwa salama mpaka uchokozi dhidi ya Ghaza utakapokoma'

Vikosi vya Ulinzi vya Yemen (YAF) vimetangaza kuwa Uwanja wa Ndege wa Ben Gurion wa Israel sasa hauko salama kwa usafiri wa anga na utaendelea kuwa hivyo hadi uchokozi wa utawala huo wa Kizayuni dhidi ya Ghaza utakapokomeshwa na vizuizi vya misaada lilivyoekewa eneo hilo la Palestina vitakapoondolewa.

Katika taarifa iliyotolewa leo Jumamosi, msemaji wa Vikosi vya Ulinzi vya Yemen Brigedia Jenerali Yahya Saree ametangaza kwamba vikosi hivyo vimeulenga uwanja wa ndege wa Ben Gurion katika eneo linalokaliwa kwa mabavu la Yaffa kwa kombora la balestiki la Palestina-2.

Kwa mujibu wa Saree, operesheni hiyo imetekelezwa "kuunga mkono watu wanaodhulumiwa wa Palestina na Muqawama wao wa kijasiri".

Msemaji wa YAF amebainisha kuwa, hiyo ni operesheni ya tatu ya shambulio la kombora la aina hiyo kutekelezwa katika muda wa saa 48 zilizopita, na akathibitisha kwamba operesheni hiyo imefikia lengo lililokusudiwa.

Mbali ya hayo, Saree ameripoti kuwa, kwa siku ya sita mfululizo, "Kikosi cha UAV" cha ndege zisizo na rubani cha Yemen kimefanya operesheni dhidi ya vyombo vya jeshi la majini la Marekani katika Bahari Nyekundu, kwa kulenga manowari zenye mfungamano na manowari ya kubebea ndege za kivita ya USS Harry S. Truman.

Brigedia Jenerali Yahya Saree amebainisha kuwa, mashambulizi hayo, ni jibu kwa uchokozi unaoendelea kufanywa na Marekani dhidi ya Yemen.

Msemaji wa YAF ametoa pongezi pia kwa wananchi wa Palestina na Muqawama wao huko Ghaza, na kusifu uthabiti wao wa kuhimili hujuma za kikatili za Wazayuni.

Operesheni mpya za Yemen dhidi ya shabaha za Israel na Marekani zimeanza tena baada ya utawala wa Kizayuni kuvunja makubaliano ya usitshaji vita yaliyodumu kwa miezi miwili huko Ghaza, ambayo yalifikiwa baina yake na Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina Hamas.

Shambulio la makombora la Yemen la leo Ijumaa ni operesheni ya nne kutekelezwa katika wiki hii kulenga maeneo ya kati ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu yaliyopachikwa jina bandia la Israel baaada ya utawala huo wa Kizayuni kuanza tena kufanya mauaji ya kimbari huko Ghaza.../

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha