22 Machi 2025 - 21:27
Source: Parstoday
Abu Obeida: Yemen imeonyesha kuwa Gaza haiko peke yake

Msemaji wa tawi la kijeshi la harakati ya Hamas amesema kuwa wananchi wa Yemen wamegharamika pakubwa kwa ajili ya kuihami Gaza, hata hivyo bado wanaendea kuwaunga mkono na kuwatetea watu wa eneo hilo.

Abu Obeida ambaye ni msemaji wa Brigedi za Izzuddun al Qassam (tawi la kijeshi la Hamas) amesisitiza kuwa kuvurumishwa makombora kutoka Yemen na Gaza kuelekea Tel Aviv kunaonyesha kuwa Gaza haiko peke yake. 

Abu Obeaida ameashiria namna watu wanavyoiunga mkono Gaza na hawasalimu amri mbele ya adui na vitisho vyake na kuwatolea mwito Waislamu na wapigania ukombozi duniani kote kushiriki katika vita vya kuihami na kuipigania al Aqsa. 

Vikosi vya Ulinzi vya Yemen vimevurumisha makombora kuelekea katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na hivyo kutatiza maisha ya Wazayuni na kuwalazimisha karibu raia milioni mbili wa Israel kukimbilia mafichoni baada ya kuakhirishwa safari za ndege. 

Mapema jana Idara ya Masuala ya Dharura ya Israel ilitangaza kuwa, Wazayuni 13 walijeruhiwa wakikimbilia mafichoni kutokana na mashambulizi ya makombora kutoka Yemen.

Abu Obeida amesisitiza kuwa Waislamu wanapasa kukamilisha mchakato wa kuiunga mkono Gaza ili kusambaratisha hatua za utawala wa Kizayuni na kuulazimisha kusimamisha vita. 

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha