26 Machi 2025 - 15:21
Source: Parstoday
'Mauaji makubwa zaidi ya watoto': Iran yalaani mauaji ya Israel na US dhidi ya watoto wa Gaza

Jamhuri ya Kislamu ya Iran imelaani vikali mauaji ya halaiki ya utawala wa Israel dhidi ya watoto wa Kipalestina katika Ukanda wa Gaza, na kuyataja kuwa ni sehemu ya sera ya iliyopangwa ya mauaji ya kimbari yenye lengo la kufuta utambulisho wa Wapalestina.

Katika ujumbe wake wa jana Jumanne kwenye mtandao wa kijamii wa X, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, Esmaeil Baqaei, alilaani mauaji ya utawala wa kivita wa Israel dhidi ya mamia ya watoto wa Kipalestina katika siku moja, na kuyataja kuwa ni mauaji makubwa zaidi ya watoto tangu Nakba ya 1948, wakati wanajeshi wa Israel waliokuwa wakisaidiwa na nchi za Magharibi, walipowafukuza Wapalestina katika nchi yao.

"Umma wa dunia sasa unatambua wazi kwamba mauaji ya watoto yanayofanywa na utawala ghasibu ni sera ya kimfumo, inayotekelezwa kwa nia ya mauaji ya kimbari ya kufuta kizazi na 'maangamizii ya kikoloni' dhidi ya watu wa Palestina," amesema Baqaei katika ujumbe huo. 

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran pia amelaani ukimya wa mashirika ya kimataifa, ukiwemo Umoja wa Mataifa, kutokana na ukatili huo wa kutisha.

Amesema: "Kuuawa na kuteswa watoto wasio na hatia wa Kipalestina kumeacha majeraha makubwa kwenye dhamiri ya ubinadamu; na kutojali kwa Umoja wa Mataifa na mashirika husika ya haki za binadamu kunazidisha majeraha hayo." 

Esmaeil Baqaei ameibebesha Marekani, mshirika mkubwa zaidi wa Tel Aviv, Uingereza, na waungaji mkono wengine wa Magharibi wa utawala huo, dhima ya kuwezesha umwagaji damu na uharibifu unaofanywa na Israel.

'Mauaji makubwa zaidi ya watoto': Iran yalaani mauaji ya Israel na US dhidi ya watoto wa Gaza

"Kwa ushirikiano kamili na uungaji mkono endelevu wa Marekani, Uingereza na baadhi ya nchi nyingine za Magharibi - na kwa kutiwa moyo na kutochukua hatua kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa -, utawala wa Israel unahisi kuwa na kinga kamili ya kuadhibiwa kwa ajili ya kuendelea kutekeleza jinai mbaya zaidi, ikiwa ni pamoja na uhalifu wa kivita, jinai dhidi ya ubinadamu na mauaji ya kimbari," amesema Baqaei.

Ujumbe huo umetolewa huku kukiwa na ripoti kwamba, mashambulizi ya anga ya Israel yameua takriban watoto 200 huko Gaza katika siku za hivi karibuni, idadi ambayo imethibitishwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF).

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha