Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahl al-Bayt (a.s) - Abna -; Swala ya Eid al-Fitr imesaliwa asubuhi ya leo kwa shauku na fahari kubwa na kwa uwepo wa mahudhutio makubwa ya Wananchi wa Taifa pendwa la Imani, Izza na Utukufu katika kila kona ya nchi. Katika Mji Mkuu wa Iran, idadi kubwa ya watu wenye nyoyo kunjufu na zilizojaa matumaini ya kupata rehema na msaada wa Mwenyezi Mungu, walijitokeza kwa wingi kushiriki katika ibada ya Swala ya Eid al-Fitr iliyoongozwa na Ayatollah Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, katika Msikiti wa Tehran na katika mitaa ya jirani na Msikiti huo.
Ayatollah Khamnenei, aliuelezea Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kuwa ni miongoni mwa neema kubwa zaidi za Mwenyezi Mungu, ni jambo la Tauhidi na ni fursa iliyotolewa na Mwenyezi Mungu kwa waja kwa ajili ya wao kujijenga kwa Ucha Mungu na kujenga ukaribu wao na Mwenyezi Mungu, pia Mwezi wa Ramadhan ni fursa ya utakaso wa nyoyo na nafsi na kutengeneza upya wa kiroho, kisha akaongeza kusema: Saumu, ukaribu na Qur'an, mikesha ya neema ya Lailatl-Qadr, ibada ya na dua ni fursa adhimu kwa ajili ya kumjenga Binadamu katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Akiashiria kuheshimu matembezi ya kitaifa na yenye maana katika Siku ya Kimataifa ya Quds katika Ijumaa ya mwisho ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani amesema: Harakati kubwa ya Taifa hili la Iran ilikuwa na jumbe tofauti tofauti kwa watu wote duniani ambao wanapaswa kufahamu na kulifahamu Taifa la Iran.
Ayatollah Khamenei katika Khutba ya pili ya Swala ya Eidul Fitri ametaja kuendelea kwa mauaji ya halaiki na mauaji dhidi ya watoto wachanga yanayofanywa na utawala wa Kizayuni huko Ghaza na Lebanon kuwa yamekuwa ni sababu ya kuleta machungu kwa Umma wa Kiislamu katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na kusema: Jinai hizo zimefanywa chini ya kivuli cha kuendelea kwa misaada na uungaji mkono wa Marekani kwa genge la uhalifu na ghasibu lilonaloikalia Palestina kwa mabavu.
Ameutaja utawala wa Kizayuni kuwa ni kikosi wakilishi cha wakoloni katika eneo la kikanda na kuongeza kuwa: Wamagharibi wanayatuhumu mara kwa mara mataifa shupavu na vijana wenye bidii (na wana jihadi) wa eneo hili kuwa ni vibaraka (vikosi vya niaba), lakini ni wazi kabisa kwamba, kundi pekee lenye uwakilishi - kibaraka - (linalofanya kazi za kijeshi kwa niaba ya mataifa koloni na uistikbari) katika eneo hili la kikanda ni utawala haram na ghasibu wa kizayuni unaoendelea na kukamilisha mpango wa nchi zilizokalia kwa mabavu eneo hili la kikanda (na kulikoloni) baada ya Vita vya Dunia (ambapo ni wakala wao anayefanya kazi hiyo) kwa kutumia njia ya mauaji halaiki na kuendesha vita vya kimbari na kufanya uvamizi na jinai mbalimbali dhidi ya nchi zingine.
Ayatollah Khamenei amelaani vikali kudharau na kupuuza kwa wadai wa haki za binadamu mbele ya mauaji ya Mashahidi takribani watoto 20,000 wa Kipalestina katika kipindi cha chini ya miaka miwili na akasema: Hata hivyo wananchi wa mataifa ya dunia yakiwemo ya Ulaya na Marekani mara tu wanapopata habari kuhusu jinai hizo, watadhihirisha hisia zao na kufanya maandamano dhidi ya Wazayuni na Marekani, na iwapo kwa hakika wananchi wa mataifa hayo watapata taarifa kamili za mambo jinsi yanavyojiri, basi watapanua zaidi malalamiko na mapingamizi yao.
Katika aina ya mukhtasari wa mambo yote yaliyotajwa, alisisitiza: Kundi hili la wahalifu, ovu na hatari kwa jinai lazima liondolewe kabisa Palestina na eneo hili la kikanda, jambo ambalo litatokea kwa matakwa ya Mwenyezi Mungu (Insha Allah), na juhudi mbalimbali katika uwanja huu (na malengo hayo) ni wajibu wa kidini, kimaadili na wa kibinadamu kwa wanadamu wote.
Akiashiria uthabiti wa misimamo ya Jamhuri ya Kiislamu kuhusu eneo hili la kikanda, Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema: Misimamo yetu ni thabiti, na uadui wa Marekani na utawala wa Kizayuni ni sawa na wa huko nyuma.
Mwishoni mwa Khutba ya pili, Ayatollah Khamenei alitoa nukta mbili muhimu kuhusu misimamo ya hivi karibuni ya vitisho ya Marekani: Kwanza, iwapo uovu wowote utafanywa kutoka nje, jambo ambalo bila shaka halina uwezekano mkubwa (kutokea), kwa hakika (waovu hao) watajibiwa kwa kupigwa kwa pigo kali sana, na pili, ikiwa adui anafikiria pengine kuzusha (fitna na) mpasuko kwa ndani, kama ilivyokuwa katika baadhi ya miaka ya nyuma, Taifa la Iran litatoa jibu kali kwa waasi (wapenzi wa fitna) kama ilivyokuwa kwa miaka hiyo.
Your Comment