Sayyid Abbas Araghchi alisema hayo jana Jumatatu na kuongeza kwamba, nchi mbili za Iran na Afghanistan zimejadiliana kwa kina pia suala la raia wa Afghanistan wanaohamia Iran kinyume cha sheria wakati wa ziara yake ya hivi karibuni mjini Kabul ambako alikutana na maafisa wa ngazi za juu wa Afghanistan.
Araghchi amesisitiza kuwa, jambo muhimu zaidi katika mchakato wa kuwarejesha wahajiri nchini kwao ni suala la usimamiaji wa zoezi hilo.
Amesema: "Tunafanya mashauriano na serikali ya Afghanistan ili kuendesha zoezi hili kwa mujibu wa sheria na utaratibu uliowekwa. Jambo hilo limejadiliwa kikamilifu na upande wa Afghanistan na kuamua kuwa mchakato huo ufanyike kwa ushirikiano wa pamoja kwa ajili ya kuwaondoa hatua kwa hatua wahamiaji hao na kwa heshima kutoka Iran na kuwapeleka Afghanistan.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran aidha amesema: "Ni muhimu sana kuhimiza kwamba upande wa pili yaani Afghanistan nao uwe na uwezo wa kuwafanya wahajiri hawa wavutike kurejea nchini kwao."
Amesema: "Hatutaki kulifanya suala la kurejea nchini kwao raia wa Afghanistan kuwa mgogoro wa kijamii kwa nchi zote mbili za Iran na Afghanistan."
Your Comment