28 Machi 2025 - 17:35
Source: Parstoday
Imam wa Swala ya Ijumaa: Maandamano ya Siku ya Quds ni dhihirisho la Tauhidi na kumpenda Mungu

Imam wa Swala ya Ijumaa ya leo katika mji wa Tehran ameashiria kushiriki kwa wingi na kwa hamas wananchi wa Iran ya Kiislamu katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Quds mwaka huu na kusema: Maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds siku zote yamekuwa dhihirisho la Tauhidi na kumpenda Mwenyezi Mungu.

Ayatullah Sayyid Ahmad Khatami amesisitiza katika hotuba ya kwanza ya ibada hiyo ya kiroho na kisiasa katika Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhan iliyofanyika sambamba na maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Quds kwamba: Matendo yote ya mwanadamu yataulizwa na Mwenyezi Mungu, na tunamshukuru Mwenyezi Mungu kuona Siku ya Quds mwaka huu imeadhimishwa kwa hamasa kubwa sawa kabisa na miaka iliyopita.  

Baada ya ushindi wa Mapinduuzi ya Kiislamu ya Iran, hayati Imam Ruhullah Khomeini (M.A) aliitangaza Ijumaa ya mwisho ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani kuwa Siku ya Quds wakati mabeberu wa dunia walipokuwa wakijaribu kuisahaulisha kadhia ya mapambano ya ukombozi wa Palestina au kulifanya suala hilo kuwa la Kiarabu, lakini hayati Imam Khomeini alisambaratisha njama hizo kwa mipango yake mikubwa. 

Imam wa Swala ya Ijumaa: Maandamano ya Siku ya Quds ni dhihirisho la Tauhidi na kumpenda Mungu

Imamu wa Swala ya  Ijumaa ya leo mjiini Tehran ameongeza kuwa: Hii leo wananchi katika miji na vijiji 900 vya Iran wameshiriki katika matembezi ya kuwatetea na kuonyesha mshikamano kwa wananchi madhulumu wa Palestina. 

Amesema watu katika nchi 80 duniani pia wameandamana kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Quds huku wakipiga nara za "Mauti kwa Israel." Matabaka mbalimbali ya wananchi huko Marekani, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani pia wameandamana leo katika Siku ya Kimataifa ya Quds; na ikhlasi ya Imam Khomeini (M.A) ndio iliyopelekea baraka zote hizi. 

Katika hotuba ya pili ya Swala ya Ijumaa ya Tehran, Ayatullah Khatami amezungumzia msingi wa kijamii na kisiasa wa Siku ya Kimataifa ya Quds na kusema: Siku ya Kimataifa ya Quds pia ina asili katika Qur'ani; Katika aya ya 120 ya Suratu Tawbah, inayoeleza kwamba hatua yoyote inayochukuliwa na waumini inawaghadhabisha makafiri. 

Amesema maandamano ya leo ya Siku ya Kimataifa ya Quds kwa hakika yanawakasirisha Netanyahu, wahalifu wa Kizayuni na Marekani, na sisi tunasema, "kufeni kwa hasira zetu."

Ayatullah Khatami pia ameashiria vitisho vya mara kwa mara vya Rais wa Marekani na kusema: "Trump ana jeni ya vitisho, na ni ajabu ni kwamba haelewi kuwa vitisho hivyo havina na havitakuwa na tija."

Akizungumzia msimamo wa wananchi wa Iran mbele ya vitisho vya Marekani na washirika wake, Imamu wa Swala ya Ijumaa ya Tehran amesoma Aya ya 173 ya Suratu Aal Imran inayosema: Wale walioambiwa na watu: Hakika watu wamewakusanyikia, kwa hivyo waogopeni! lakini hayo yakawazidishia imani, wakasema: Mwenyezi Mungu anatutosha, na Yeye ndiye Mbora wa kutegemewa. 

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha