28 Machi 2025 - 17:43
Source: Parstoday
Kilele cha ukatili wa Israel; Waliouawa shahidi Gaza wapindukia 50,200

Jeshi katili la Israel ambalo lilianzisha mashambulizi mapya ya anga katika Ukanda wa Gaza mnamo Machi 18, limeendelea kupuuza miito ya jamii ya kimataifa ya kukomesha ukatili wake katika ukanda huo; ambapo mpaka sasa limeshaua shahidi Wapalestina karibu 900 na kujeruhi wengine karibu 2,000.

Wapalestina saba wameuawa shahidi katika shambulizi jipya zaidi la Wazayuni kwenye soko lenye shughuli nyingi katikati mwa Gaza, huku makumi ya watu wakiuawa katika wimbi la hujuma hizo katika eneo hilo lililo chini ya mzingiro katika muda wa saa 24 zilizopita.

Takriban Wapalestina 40 wameuawa shahidi katika mashambulizi hayo mapya ya Israel yaliyofanywa kote Ukanda wa Gaza, na hivyo kufanya idadi ya vifo kutokana na mashambulizi ya Israel tangu Oktoba 2023 kupindukia ya 50,200.

Taarifa ya Wizara ya Afya ya Gaza ilisema jana Alkhamisi kwamba, watu 82 zaidi waliojeruhiwa katika saa 24 zilizopita wanatibiwa hospitalini. "Waathiriwa wengi bado wamenasa chini ya vifusi na barabarani kwani waokoaji hawawezi kuwafikia," taarifa ya wizara hiyo imeongeza.

Hata hivyo, Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Serikali ya Gaza imesasisha idadi ya waliouawa shahidi kuwa zaidi ya 61,700, ikisema maelfu ya Wapalestina waliotoweka chini ya vifusi wanakisiwa kuwa wameaga dunia.

Katika moja ya mashambulizi yake ya hivi punde zaidi katika mji wa Gaza, ndege za Israel zilishambulia nyumba moja katika eneo la al-Saftawi na kuua Wapalestina saba. Utawala huo katili unaendelea jinjai hizo Gaza huku ukipuuza makubaliano ya kusitisha mapigano na kubadilishana wafungwa na mateka yaliyofikiwa Januari mwaka huu.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha