28 Machi 2025 - 17:45
Source: Parstoday
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Glasgow wagoma kula katika kuihami Gaza

Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha serikali cha Glasgow, Scotland wamefanya mgomo wa kula wakilalamikia ushirikiano wa chuo hicho na makampuni yanayotengeneza silaha kwa ajilii ya utawala wa Kizayuni wa Israel.

Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Glasgow huko Scotland ambao ni wanachama wa Taasisi ya Kupigania Haki za Palestina yaani Justice fo Palestine Society wamewakosoa wakuu wa chuo hicho na kuwataka wasitishe ushirikiano na makampuni hayo ya silaha kwa ajili ya Israel. 

Taasisi hiyo ya kupigania haki za Palestina katika Chuo Kikuu cha Glasgow ambayo imerusha video ya wanachama wake katika mitandao ya kijamii wanaoendelea na mgomo wa kula kwa ajili ya kuihami Palestina, imetangaza kuwa Chuo Kikuu cha Glasgow kimewekeza pauni milioni 6.8 katika kampuni ya uundaji silaha ya BAE Sysytem ambayo ni kampuni kubwa zaidi ya uundaji silaha na zana za kijeshi barani Ulaya. 

Gazeti la Glasgow Times limeandika kuwa: Watetezi na wale wote wanaoiunga mkono Palestina wanasema kuwa Chuo Kikuu cha Glasgow kinashiriki katika uhalifu na jinai za kivita dhidi ya Wapalestina kwa hatua yake ya kuwekeza katika kampuni hiyo ya silaha inayounda silaha kwa ajili ya Israel.

Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Glasgow wagoma kula katika kuihami Gaza

Maelfu ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza wameuawa hadi sasa katika kampeni ya mauaji ya kimbari yanayoendelea kufanywa na Israel huko Gaza. 

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha