Sayyid Abdul-Malik al Houthi ameashiria katika hotuba yake ya jana Ijumaa kwamba katika baadhi ya siku Marekani inatekeleza mashambulizi zaidi ya 90 na kusisitiza kuwa: Mashambulizi ya Marekani licha ya kushtadi hivi karibuni lakini hayajakuwa na athari hasi kwa nguvu na uwezo wa kijeshi wa Yemen.
Al Houthi amesema: Mashambulizi ya Marekani yameshindwa kusitisha operesheni za kijeshi za kuwaunga mkono wananchi wa Palestina, na pia kuzilinda meli za utawala wa Kizayuni katika Bahari Nyekundu, Ghuba ya Aden na Bahari ya Oman.
Wakati huo huo, Muhammad al Bukhaiti mwakilishi wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Ansarullaj jana usiku alisisitiza kuwa: Hakuna haja ya kufanya mazungumzo ya moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja na Marekani.
Al Bukhaiti pia ameongeza kuwa: "Operesheni zetu zitasimama pale makubaliano ya kusitisha vita dhidi ya Gaza yatakapotekelezwa".
Katika kuuhami utawala wa Kizayuni na katika juhudi za kuvunja mzingiro wa majini uliowekwa na Yemen dhidi ya utawala ghasibu; Marekani inatekeleza mashambulizi dhidi ya raia wa Yemen ambapo hadi sasa makumi ya Wayemen wameuawa shahidi na kujeruhiwa
342/
Your Comment