13 Aprili 2025 - 00:42
"Tumbo ndio Makao Makuu ya Magonjwa Mengi ya Binadamu"

Mtume (saww) ametuambia kuwa "fungeni mpate afya". Na Madaktari wana kitengo maalum cha matibabu kwa kutumia funga, yaani kuna maradhi maalum katika magonjwa ambayo Binadamu tunaugua tiba yake ni kufunga.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA - “Mtume Muhammad (saww) anatuambia kuwa tumbo ndio makao makuu ya magonjwa, yaani: Magonjwa mengi ya Binadamu chanzo chake ni tumboni.

Kwa hiyo tuangalie tunakula nini na tunakula vipi, lakini yote kwa ujumla, Mtume (saww) ametuambia kuwa "fungeni mpate afya". Na madaktari wana kitengo maalum cha matibabu kwa kutumia funga, yaani kuna maradhi maalum katika magonjwa ambayo Binadamu tunaugua tiba yake ni kufunga. Kwa mfano: Ugonjwa wa kwanza ni uzito au ugonjwa wa moyo kama vile moyo una mafuta mengi au moyo umekuwa mkubwa.

Sasa, ili upate faida hizi angalia unafuturu au unakula nini, watu wanakosea katika funga, unamkuta mtu wakati wa futari anakula vyakula vingi sana mpaka tumbo linamuuma! hata kuinuka alipo kaa anashindwa! Hiyo ni hatari sana kwake.

Hayo yamesemwa na kubainishwa na Sheikh Kiza Mussa Kiza kwenye kipindi cha Maswali na Majibu kinachorushwa Mubashara kupitia IBN TV Africa.

Your Comment

You are replying to: .
captcha