12 Aprili 2025 - 15:44
Kushindwa kwa Marekani nchini Yemen kumezusha wasiwasi miongoni mwa nchi za Kiarabu. Nini kitatokea ikiwa San'a itakuwa Mamlaka yenye Nguvu Kikanda?

Kwa kuzingatia chaguzi ndogo za Amerika, mashaka yameongezeka miongoni mwa maadui wa Yemen katika nchi za Ghuba ya Uajemi, na hii imefanya kazi ya vyombo vyao vya habari - ambavyo vinaendana kikamilifu na (riwaya) simulizi ya Marekani na Israel - kuwa ngumu; Hadi wanakimbilia kuwatuhumu “Ansarullah” kwa kutumia vita vibaya.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul Bayt (a.s) - ABNA -, Marekani iko katika hali ngumu katika vita vyake visivyo na usawa na Yemen. Vita hivyo vimekuwa kashfa kwa sababu havina mkakati wa wazi, zaidi ya msisitizo wa Rais wa Marekani Donald Trump kwa kile anachokiita hatua ya haraka na bila kuchoka kwa karibu pande (nyanja) zote. Kulingana na jarida la Amerika "The Atlantic," vita hivi vinaweza kuwa na matokeo mabaya ikiwa serikali ya Amerika haitabadilisha mkondo wake.

Hofu ya kushindwa uvamizi huo wa Marekani dhidi ya Yemen, imezitia wasiwasi duru nyingi za maamuzi katika nchi za Magharibi na nchi za Kiarabu za Ghuba ya Uajemi. Wasiwasi huu unaonyeshwa wazi katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii na unajadiliwa miongoni mwa maafisa wa Marekani na Waarabu. Hasa kwa vile kushindwa kokote kutaifanya Yemen kuwa na nguvu zaidi kijeshi na kisiasa na kuwa na misingi imara zaidi kuliko hapo awali.

Katika wiki za hivi karibuni, imedhihirika kwa kila mtu kwamba madai ya kijasusi ya Marekani ya kupata mafanikio katika kusasisha maeneo ya kushambulia na udhibiti wake ndani ya Yemen yalikuwa ni madai matupu, na uwongo wake wa wazi wa madai ya kuwauwa viongozi wakuu wa harakati ya Ansarullah ulifichuliwa hadharani. Kufuatia hili, mashine ya propaganda ya Marekani ilirejea tena kwenye simulizi (riwaya) kwamba Ansarullah inafurahia (inajivunia) faida ya kuwa katika maeneo ya mbali ya milima na kwamba sehemu kubwa ya safu yake ya kijeshi inawezekana kuwa salama dhidi ya mashambulizi.Pia ilidaiwa kuwa jeshi la Yemen si jeshi la kawaida na halina miundombinu mikubwa na mali ya kijeshi na kwamba ingelemazwa uwezo wake wa kijeshi ikiwa itapigwa kwa mabomu.

Jeshi la Yemen limefanikiwa kuendeleza mbinu zake za mapambano na mbinu za kijeshi kwa mujibu wa vitisho vya kudumu na vinavyojitokeza, hivyo inaendelea na mipango yake ya kijeshi ya kwa wepesi na kwa kasi ya hali ya juu. Jeshi hili pia linatumia mbinu za kisasa za ulinzi tulivu kabisa, kwa upande wa ardhini na za kiufundi zaidi, na lina uwezo wa hali ya juu katika kuficha, kujificha, kufanya harakati za haraka na kujihifadhi katika maeneo yaliyotawanyika na kwenye ardhi ya eneo tata. Kwa kuongeza katika hilo, Harakati ya Ansarullah ina rasilimali watu ambayo daima iko katika uwanja wa teknolojia na matumizi akili ya bandia / Artificial intelligence (AI) katika nyanja zote. Hili ndilo jambo ambalo Donald Trump pia amekiri na kusema kuwa, Wahouthi (Ansarulllah) wanamiliki silaha za hali ya juu katika uwanja wa ndege zisizo na rubani na makombora, ambayo mengi yake yanatengenezwa nchini Yemen.

Kwa hivyo, Washington ilijikuta ikikabiliwa na aina ya silaha na mbinu ambazo zilikuwa tofauti na vile jeshi la Merika lilizoea. Vita hivi havifanani na vita vya kawaida vya jeshi wala haviingii kikamilifu katika mfumo wa vita vya msituni. Kwa hivyo, Amerika inakabiliwa na adui asiyeonekana na ambaye yupo kama kivuli na ambaye ana uwezo uliozingatia na wakati huo huo usiozingatia, ambaye hufanya shughuli zake kwa njia iliyoratibiwa, na hufanya kulingana na maagizo ya hapo awali, na, ikiwa ni lazima, hufanya maamuzi kulingana na hali ya uwanjani namna ilivyo.

Jeshi la Yemen limeweza na kufanikiwa kuishughulisha na kuichanganya mashine kubwa ya kijeshi ya Marekani yenye shughuli nyingi za kijeshi, licha ya matumizi makubwa ya moto mkali (nguvu kubwa mashambulizi) na matumizi ya silaha za kisasa - ambazo ni za kizazi cha juu cha sialaha ya Marekani (lakini bado wamefeli mbele ya Jeshi la Yemen linalopambana kwa kutumia mbinu za hali ya juu za kijeshi). Kuhusiana na suala hili, Wayemen wameweza kufikia hili kupitia hali yao ngumu (uvumilivu na ustahmilivu), eneo lao la kijiografia linawabeba, na matumizi ya silaha zinazotishia urambazaji katika Bahari Nyekundu au kulenga utawala wa Kizayuni kwa makombora mara kwa mara.

Utata huu uliotolewa na Jeshi la Yemen katika uwanja wa mapambano dhidi ya Marekani,  umepunguza sana kasi ya maendeleo ya Marekani, na kulazimisha Ikulu ya Marekani kuzingatia hali ngumu zaidi ya mashambulizi badala ya kutegemea chaguzi za haraka. Ikiwa jeshi la Marekani litaamua kupanua mashambulizi, litakabiliwa na kuendelea kwa Wayemen na watakuwa na benki tupu ya maeneo ya shabaha zao za kushambulia, na ni shabaha zile zile tupu zinazojirudia rudia za kijeshi ambazo zimekuwa zikishambuliwa zitashambuliwa na kulengwa mara nyingi hapo awali kupitia Marekani au Saudi Arabia; na wakati mwingine wanajikuta wanaishia kufanya mashambulizi kwenye maeneo ya kiraia ambayo husababisha tu mauaji ya raia wasio na hatia na ni mashambulizi ambayo hayana faida yoyote ya kijeshi kwa Washington.

Uamuzi wa kupanua mashambulizi ya Marekani dhidi ya Yemen pia unahitaji miezi mingi ya kazi ya kijasusi, kiufundi na uwanja na hata binadamu, na hii itaongeza muda wa vita zaidi ya makadirio ya Marekani. Zaidi ya hayo, upanuzi huu hauendani na mkakati uliotangazwa wa Marekani wa kumaliza vita na kudai kujitahidi kuleta amani katika Mashariki ya Kati; Na hili huenda likailazimu Marekani kuulazimisha utawala wa Kizayuni kusitisha hujuma dhidi ya Ghaza. Washington sasa imenaswa kati ya chaguzi hizi mbili - na zote mbili ni za gharama kubwa na chungu kwa heshima na uaminifu wake ulimwenguni.

Kwa kuzingatia hali hiyo, Wamarekani wamepokea nasaha kutoka kwa washirika wao katika Ghuba ya Uajemi kuhusiana na ulazima wa kutatua haraka suala la Yemen, hasa kwa kuhofia kwamba kuendelea vita katika Bahari Nyekundu kutawapa viongozi wa harakati ya Ansarullah umaarufu wa ziada wa kieneo baina ya Waarabu na Waislamu, na kuwageuza kuwa kigezo kilichoenea na kisichoweza kudhibitiwa kwa ajili ya kukusanya na kuhamasisha vikosi zaidi, na kuwajengea msimamo wa kieneo na kimataifa ambao utakuwa mgumu kuudhibiti na kuushughulikia katika siku zijazo; Hii ni pamoja na kwamba wanajulikana kuwa dola kuu la Kiarabu katika kukabiliana na utawala wa Marekani na kusimama kidete dhidi ya utawala wa Kizayuni.

Kwa kuzingatia chaguzi ndogo za Amerika alizobakia nazo mkononi kuikabilia Yemen, mashaka yameongezeka miongoni mwa maadui wa Yemen katika nchi za Kiarabu za Ghuba ya Uajemi, na hii imefanya kazi ya vyombo vyao vya habari - ambavyo vinaendana kikamilifu na (riwaya) simulizi ya Marekani na Israel - kuwa ngumu; Hadi wanakimbilia kuwatuhumu “Ansarullah” kwa kutumia vita vibaya.

Kinyume chake, nchi za Kiarabu za Ghuba ya Uajemi zimekusanya vikosi vyao vya wakala ndani ya Yemen ili kutengeneza fursa ya kweli dhidi ya Ansarullah. Hivi sasa, juhudi nyingi zinaendelea kukomesha mpasuko wa ndani na kuimarisha uanzishwaji wa kijeshi chini ya uungaji mkono wa muungano wa Waarabu. Ili kuweza kuchukua nafasi kulingana na mpango tofauti wa hapo awali, kwa kisingizio kuwa wanajiandaa kusonga mbele kuelekea San'a, na haya yanajiri baada ya jeshi la Yemen kuanza kuonyesha dalili za kuchakaa na kumomonyoka kutokana na mashambulizi ya Marekani kuanza kuonekana.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha