4 Mei 2015 - 18:19
 Wapinzani wakataa kujiunga na serikali ya Netanyahu Israel

Waziri wa mambo ya nje wa Israel asiyekhofia kusema chochote Avigdor Lieberman amesema kwamba chama chake ya Yisrael Baitenu hakitojiunga na serikali ya mseto inayoundwa na waziri mkuu Benjamin Netanyahu.

Waziri wa mambo ya nje wa Israel asiyekhofia kusema chochote Avigdor Lieberman amesema kwamba chama chake ya Yisrael Baitenu hakitojiunga na serikali ya mseto inayoundwa na waziri mkuu Benjamin Netanyahu. Taarifa hizo zimetangazwa na vyombo vya habari nchini humo.Tangazo hilo la kushtukiza limekuja siku mbili kabla ya muda wa mwisho uliowekwa kwa Netanyahu kuwasilisha serikali yake mpya aliyotarajia itakuwa ya mrengo wa kulia ikijumuisha watu wanaozingatia dini. Lieberman amenukuliwa katika tovuti ya gazeti la  Haaretz akisema wamefikia uamuzi wa pamoja wa kutojiunga na serikali hiyo ya mseto.Chama cha Liberman chenye msimamo mkali kinachowapinga waarabu kilishinda viti sita katika uchaguzi wa mwezi Machi na kilitarajiwa  kujiunga na chama cha Netanyahu cha Likud  katika serikali inayoundwa na vyama sita.Hata hivyo hatua ya Lieberman haitomzuia Netanyahu kuunda serikali bali itaipunguzia serikali yake wingi wa viti bungeni, kwa kuambulia viti 61 tu badala ya 67 ambavyo ingevipata katika bunge lenye viti 120.