10 Mei 2015 - 12:46
Maelfu ya wananchi wakimbia mapigano Sudan Kusini

Maelfu ya watu wamekimbia mapigano makali katika jimbo la kaskazani la Sudan Kusini la Unity na mashirika ya misaada yamewaondoa wafanyakazi wake katika eneo hilo.

Maelfu ya watu wamekimbia mapigano makali katika jimbo la kaskazani la Sudan Kusini la Unity na mashirika ya misaada yamewaondoa wafanyakazi wake katika eneo hilo. Taarifa hizi ni kwa mujibu wa Kamati ya Kimataifa ya Shirika la Msalaba Mwekundu na mashirika mengine.

Msemaji wa jeshi la serikali ya Sudan Kusini Philip Aguer amethibitisha kutokea mapigano hayo  katika Jimbo la Unity lakini msemaji wa waasi hakuweza kupatikana mara moja kuelezea kuhusu taarifa hizo.

Madaktari wasio na mipaka wamesema wameifunga hospitali katika mji wa Leer kutokana na  ripoti juu ya   uwezekano  wa  kufanyika mashambulizi. Mgogoro wa kisiasa nchini Sudan Kusini ulianza mwishoni mwa mwaka 2013 baada ya kuzuka mapigano kati ya wanajeshi watiifu kwa Rais Salva Kiir na ushirika wa waasi wanaomtii aliyekuwa makamu wake Riek Machar.