10 Mei 2015 - 13:30
Waziri wa mafuta wa Iran nchini Ujerumani

Waziri wa mafuta wa Iran siku ya Alhamisi alisafiri kwenda nchini Ujerumani kwa lengo la kuonana na waziri wa uchumi na maendeleo (Gabriel) pamoja na waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani (Frank-Walter)

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: BijanNamdarZangeneh ameonana na msaidizi wa Kansela wa Ujerumani na waziri wa uchumi katika jengo la wizara ya uchumi nchini Ujerumani, na baada ya kikao hicho alishiriki katika kikao cha kimataifa cha Nishati mwaka 2015 mjini Berlin na alijibu maswali mbalimbali ya waliohudhuria kikao hicho.

Kwamujibu wa ripoti hii waziri huyo wa mafuta wa Iran ameonana na wakuu wa mashirika makubwa wa biashara ya mafuta nchini humo, na baada ya hapo alionana na waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani nchini humo.

Safari ya waziri huyo nchini Ujerumani imetokea baada ya serikali ya Ujerumani kuamua kukuza uhusiano wake na Iran baada ya makubaliano ya mpango wa nyuklia wa Iran.