Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: Majiidi Saajid amesema meli hiyo imebeba tani 2100 ya michele, unga wa ng`ano na vyakula vingine mbalimbali ikiwemo na madawa, vilevile meli hiyo imechukua waokoaji 40 au 60 kutoka shirika la uokoaji Iran (mwezi mwekundu).
Aidha amesisitiza kuwa misaada hiyo imetolewa na taasisi na vikundi vya kijamii (NGO) hivyo kufanikiwa kukusanya kiasi cha madawa, mablangeti na vyakula mbalimbali kwaajili ya wananchi wa Yemen.
Vikundi hivyo vya kijamii vimeeleza sababu za kutuma misaada hiyo nchini humo kuwa ni suala la kuwasaidia wananchi wa Yemen waliko katika hali mbaya nchini humo.