27 Juni 2015 - 21:27
Mazungumzo kuhusu Nyuklia ya Iran yaendelea

Marekani na washirika wake wamekuwa wakijitahidi kupotosha makubaliano hayo kwa kuingiza mashart yao binafsi, jambo linalopingwa vikali na serikali ya jamhuri ya kiislamu ya Iran.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry na mwenzake wa Iran Javad Zarif wanakutana leo mjini Vienna kwa mazungumzo ya mpango wa nyuklia wa Iran. Pia mawaziri wa mambo ya nje wa Uingereza, China, Ufaransa, Urusi pamoja na Ujerumani wanatarajiwa kuungana nao katika mazungumzo hayo mwishoni mwa juma.

Nchi hizo 6 zenye nguvu zaidi duniani zinaitaka Iran kupunguza shughuli zake za kinyuklia ili badala yake iondolewe vikwazo ilivyowekewa. Hakuna uhakika iwapo Iran itakubaliana na matakwa hayo. Ingawa siku ya mwisho ya kufikiwa makubaliano kamili ni Jumanne, kuna uwezekano wa mazungumzo hayo kuongezwa muda. Zarif amesema makubaliano yatafikiwa iwapo upande wa nchi hizo 6 hautotoa masharti ya kupindukia.

Marekani na washirika wake wamekuwa wakijitahidi kupotosha makubaliano hayo kwa kuingiza mashart yao binafsi, jambo linalopingwa vikali na serikali ya jamhuri ya kiislamu ya Iran.

Mwisho wa habari/ 291