Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: sheikh wa Azhar aliyasema hayo katika mazungumzo yake ya mwezi mtukufu wa Ramadhani katika televisheni ya Misri, huku akiashiria kuwa kuwatusi masahaba si jambo sahihi na lapaswa kukoma swala hilo, pia kwa upande mwingine alisema kuwa kuna vikundi vingine vya wafuasi wa madhehebu ya Sunni wenye kasumba tunaviona vinafanya vitendo visivyo sahihi vya kuwakafisha mashia na kuwaita kuwa ni marafidhiy, kitu ambacho kinasababisha mvutano baina ya pande mbili hizo jambo ambalo halifai kutendwa.
Sheikh Ahmad Tayib amesisitiza kuwa maulama wa pande zote mbili wanapaswa kukuza fungamano lao ili kupunguza tafauti ziliopo baina yao.
Aidha alisisitiza kuwa lengo letu ni kutafuta umoja wa Kiislamu nakuepuka kufarakisha Waislam huku akithibitisha kuwa wanazuoni wa Azhar hawana fikra ya kuleta mtafaruku katika jamii ya Kiislamu hawausiki na vitendo hivyo.
Naye alimalizia kusema kuwa suala la kuwatusi masahaba lazima lisitishwe, kwani endapo litaendelea kamwe hakutapatikana umoja na maelewano baina ya Waislamu katika jamii zao.
mwisho wa Habari/290