Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Chama cha CDU katika jimbo muhimu la Berlin nchini ujerumani kimekataa kata kata uanzishwaji wa sheria za jinsia moja. Wanachama wote 12,500 wa chama hicho katika mji huo mkuu walitakiwa kushiriki kwenye kura ya maoni juu ya pendekezo hilo, wakijibu suali la endapo wapenzi wa jinsia moja waruhusiwe kuoana. Asilimia 45 ya wanachama wa chama hicho kinachoongozwa na Kansela Angela Merkel wa Ujerumani wamesema hapana, kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa CDU, Kai Wegner. Mjadala wa ama au la Ujerumani iruhusu ndoa za jinsia moja kama yalivyo mataifa mengine ya Magharibi umeligawa taifa hili lenye nguvu kubwa zaidi kiuchumi barani Ulaya, hadi kwenye serikali ya mseto inayoongozwa na muungano wa CDU/CSU pamoja na chama cha SPD.
Mwisho wa habari/ 291