11 Agosti 2015 - 10:50
Uingereza yamuachia huru mkuu wa upelelezi wa Rwanda

Mahakama nchini Uingereza imetupilia mbali kesi dhidi ya mkuu wa upelelezi wa Rwanda, Jenerali Emmanuel Karenzi Karake.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Mahakama nchini Uingereza imetupilia mbali kesi dhidi ya mkuu wa upelelezi wa Rwanda, Jenerali Emmanuel Karenzi Karake. Mahakama hiyo imesema haina mamlaka kumhukumu jenerali huyo, ambaye anatafutwa na Uhispania kwa tuhuma za ugaidi. Serikali ya Uhispania inadai Karake aliamuru mauaji dhidi ya wahispania 9, katika kile kilichoelezwa kuwa ulipizaji kisasi kwa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994. Idara ya uendesha mashitaka ya Uingereza imesema imeiacha kesi hiyo, kwa sababu sheria iliyotumiwa haiwahusu watu wasio wakazi wa Uingereza. Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Rwanda Louise Mushikiwabo ameelezea kufurahishwa kwake na hatua hiyo itakayomruhusu Jenerali Karake kurudi nyumbani Rwanda, akikiita kisa cha kukamatwa kwake mchakato dhalimu, ambao haukupaswa kuwepo.

Mwisho wa habari/ 291