5 Septemba 2015 - 15:17
Mfalme wa Saudi Arabia wakutana na Rais Obama mjini Washingto

Mfalm wa Saudi Arabia (Salman bin Abdilaziz) ameonana na Rais wa Marekani Baraka Obama na kufanya mazungumzo mjini Washington

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: mfalme Salman aliwasili jana Ijumaa nchini Marekani ambapo ndio safari yake kwanza nchini humo baada ya kupata cheo cha ufalme wa Saudi Arabia, naye baada ya kufika mjini Washington alionana na Rais wa nchi hiyo mheshimiwa Baraka Obama nakufanya mazungumzo kati yao.
Rais wa Baraka Obama ndiye aliyemuitisha mfalme huyo nchini humo, pande hizo mbili katika mazungumzo yao walizungumzia masuala yanayohusu mabadiriko ya ukanda wa mashariki ya kati hasa kuhusu vita iliopo nchini Syria, machafuko ya Yemen, mpango wa nyuklia wa jamhuri ya kiislamu ya Iran na harakati za kikundi cha kigaidi cha Daesh.
Katika mazungumzo hayo mfalme wa Saudi Arabia amesema kuwa Saudi Arabia itaendelea kushirikiana na serikali ya Marekani katika kuleta amani na utulivu katika nchi za mashariki ya kati.
Rais Baraka Obama naye amesema kuwa serikali ya Marekani nayo itadumisha na kuenedeleza ushirikiano wetu na Saudi Arabia katika kupambana na magaidi duniani ikiwemo kukisambaratisha kikundi cha kigaidi cha Daesh.
Mazungumzo hayo yamejiri katika hali ambayo utawala wa Saudi Arabia na Marekani zinatuhumiwa kuvisaidia vikundi vya kigaidi kwa kuwapa silaha na misaada mingine ya kivita hususan kikundi cha kigaidi cha Daesh.

Mwisho wa Habari/290