11 Septemba 2015 - 18:30
Mwanamke wa kiiraq apinga ombi la Rais wa Ufaransa

Francois Hollande (Rais wa jamhuri ya Ufaransa) baada ya kuhudhuria katika maonyesho yaliofanyika mjini Paris Ufaransa alioonana na binti mmoja mfuasi wa dini ya Izadi kutoka nchini Iraq nakutoa umbi lake la kumtaka binti huyo abaki nchini humo umbi ambalo dada huyo hakulikubali

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: maonyesho hayo yalifanyika mjini Paris yalikuwa na Anuani hii kuwa (vita nchini Iraq na mashariki ya kati) ambayo yalihudhuriwa na baadhi ya waathirika wa vita hiyo nchini Paris.
Maonyesho hayo yalitembelewa na Rais wa nchi hiyo Francois Hollande akiwa kama mgeni Rasmi, Rais huyo pia alizungumzia suala la wakimbizi wanaotoka katika nchi zilio athirika na vita hizo.
Aidha katika maonyesho hayo Rais Francois Hollande alionana na (Jinani Badil) ambaye ni binti kutoka Iraq mfuasi wa dini ya Izadi ambaye ameandika kitabu kwajina la (kikundi cha kigaidi cha Daesh na kuwateka wanawake).
Rais huyo baada ya kuangalia na kupitia kitabu hicho alisema kumwambia Jinani Badil kuwa kitabu chako kimenivutia sana na matumaini yangu kuwa hatutashuhudia matukio kama haya dhidi ya wanawake ulimwenguni kote.
Aidha akisisitiza kuwa nchi yake iko tayari kuwapokea wakimbizi wanaotoka katika nchi ziliokuwa ba vita amesema: tufikishie ujumbe wetu wa amani kwa watu wa Kurdistan ya Iraq na waambie kuwa Ufaransa daima iko pamoja nao katika kupambana na kikundi cha kigaidi cha Daesh.
Rais huyo mwisho wa mazungumzo yake na dada huyo wa Kiiraq alimuomba abaki nchini Ufaransa, ili aendeleze harakati zake za uandishi nchini humo, ama dada huyo alitoa jawabu la ombi hilo kwakusema: kukimbia nchini hakutatui matatizo ya Iraq, njia pekee ya kuiokoa Iraq ni kubaki ndani ya nchi na kutafakari jinsi gani tatizo hilo litatatuliwa.
Aidha dada huyo alibainisha kuwa yeye yupo kwaajili ya kuwasaidia wanawake waliofungwa na wanachi wa nchi hiyo alimwambia Rais huyo kuwa: ninachokiomba kwako kuhusu wananchi wa nchi yangu ni kwamba musizidishe kuwashawishi kukimbia nchi, kwa maana kukimbia na kulihama taifa si njia sahihi ya utatuzi wa matatizo yaliopo nchini Iraq kwa sasa.
Dada huyo akielezea undani wa kikundi cha kigaidi cha Daesh alifafanua kuwa: mimi miezi 3 nilikuwa msituni na kikundi cha kigaidi cha Daesh, ambapo kitabu hichi ni tija ya yale nilioshuhudia na kufanyiwa nikiwa mateka katika kikundi hicho.
Aidha alisema: kipindi chote nilipokuwa nimetekwa na kikundi hicho nimeshuhudia matukio yakinyama mengi sana yanayofanwa na kikundi hicho cha kigaidi kwani magaidi hao hawakuacha njia yeyote ya kuadhibu ila waliitumia kutuadhibu.

Mwesho wa Habari/290