15 Septemba 2015 - 09:32
Serikali ya Hungary yafunga kivuko muhimu cha wakimbizi

Hungary imetumia waya wa seng'eng'e kukifunga kivuko muhimu cha wakimbizi na Serbia na kuonya kuhusu enzi mpya ya kuwarejesha makwao wakimbizi.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Hungary imetumia waya wa seng'eng'e kukifunga kivuko muhimu cha wakimbizi na Serbia na kuonya kuhusu enzi mpya ya kuwarejesha makwao wakimbizi. Waziri mkuu wa Hungary Victor Orban ameonya kwamba watu wanaoingia nchi mwake kutoka Serbia ambayo si mwanachama wa Umoja wa Ulaya watakabiliwa na sheria mpya za kukataliwa na kurudishwa nchini kwao.

Huku mkataba wa Schengen wa miaka 20 ukikabiliwa na shinikizo la kusambaratika Austria na Slovakia zimesema zitaiga mfano wa Ujerumani katika kudhibiti mipaka yao na kukagua hati za wakimbizi wanaotaka kuingia katika mataifa hayo. Poland imesema itafakari kuchukua hatua kama hizo huku Uholanzi ikisema itaimarisha doria katika maeneo ya mipaka yake.

Mwisho wa habari/ 291