Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: makamu wa pili wa kiongozi wa kikundi cha kigaidi cha Daesh (Abubakari Al Baghdaidy) ameuwawa katika mashambulio ya anga yaliofanywa na majeshi ya Iraq nchini humo.
Vyombo vya habari mbalimbali muda punde vimetanganza habari hiyo vikinukuu kutoka kwa vyanzo vya habari vya majeshi ya Iraq ambapo vimethibitisha kuangamia kwa makamu wa pili wa kikundi hicho cha kigaidi.
Aidha kwamujibu wa habari hii “Aaswi Ali Nasir” makamu wa pili wa Abubakari Albaghdadiy (kiongozi wa kikundi cha kigaidi cha Daesh) ameangamia katika mkoa wa Anbar nchini Iraq.
Kutokana na maelezo ya vyanzo makini vya kijeshi nchini Iraq vyathibitisha kuwa kiongozi huyo ameangamia baada ya mashambulizi makali yaliofanywa na ndege za Iraq katika sehemu ya Parwaneh iliopo katika wilaya ya Haditha magharibi mwa mkoa wa Anbar nchin Iraq.
Inasemekana kuwa mnamo tarehe 12 mwezi Desemba mwaka jana wizara ya mambo ya ndani ya Iraq ilitangaza kujeruhiwa kwa makamu wa kwanza wa kiongozi huyo wa kikundi cha kigaidi cha Daesh na kuangamia viongozi wajuu 15 katika mashambulio maalumu yalifanywa na jeshi la anga katika makazi ya viongozi hao ambao walikuwa sehemu ya “Akjazirah” iliopo katika mipaka ya Syria ya Iraq.
mwisho wa Habari/290