17 Februari 2016 - 16:36
Serikali ya Syria yaruhusu kuingizwa msaada wa raia

Serikali ya Syria imetoa ruhusa ya misaada ya kibinadamu kupelekwa katika maeneo saba yaliyozingirwa na magaidi wanaoungwa mkono na Marekani na washika wake.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Serikali ya Syria imetoa ruhusa ya misaada ya kibinadamu kupelekwa katika maeneo saba yaliyozingirwa na magaidi wanaoungwa mkono na Marekani na washika wake.

Hayo ni katika siku ambayo serikali ya Uturuki ambayo inasaidia magaidi imetowa wito wa kuanzishwa operesheni ya jeshi la nchi kavu katika nchi hiyo jirani iliyoharibiwa na vita.

Misafara ya Umoja wa Mataifa inayopeleka misaada kwa maelfu ya Wasyria waliokwama katika miji iliyozingirwa na magaidi wanaoungwa mkono na Uturuki na Marekani imeanza leo, ikielekea katika miji kadhaa ukiwemo Madaya ambako watu kadhaa wanaaminika kufa kutokana na njaa.

Akizungumza mjini Damascus, mjumbe wa Umoja wa Mataifa Staffan de Mistura amesema misafara ya msaada itatumwa leo katika kile kitakachokuwa ni mtihani wa ikiwa pande zinazozozana zitaruhusu kuingia misaada hiyo ya kiutu.

Takribani watu nusu milioni nchini Syria wako katika maeneo yaliyozingirwa, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, baada ya karibu miaka mitano ya vita vya vinavyochochewa na Marekaim Saudia arabia uturuki na washirika wako kwa lengo la kuiangusha serikali halali ya  syria.

Shirika la Hilali Nyekundu limesema misafara ya kwanza itaelekea katika vijiji vilivyozingirwa na magiadi wanauongwa mkono na Mareknai na washirika wake vya Fuaa na Kafraya katika upande wa Kaskazini, na Madaya na Zabadani, ambavyo vimezingirwa na jeshi ya Syria katika hatua za kuwadhibiti magaidi.

Lakini mashambulizi ya makombora kwenye hospitali tano na shule mbili kaskazini mwa Syria ambayo Umoja wa Mataifa ulisema yaliwauwa watu 50 wakiwemo watoto, yamepunguza matumaini ya kutekelezwa mpango wa kusitisha mapigano uliofikiwa na mataifa yenye nguvu duniani mjini Munich wiki iliyopita. Chini ya makubaliano hayo, duru mpya ya mazungumzo itaandaliwa Geneva Februari 25.

Rais Barack Obama wa Marekani anasema itakuwa vigumu kuutekeleza mpango huo wa kuweka chini silaha ikiwa Urusi itaendeleza mashambulizi yake dhidi ya magidi hao wanaodhaminiwa na Marekani "Ukweli kwamba Putin hatimaye aliyapeleka majeshi yake na ndege zake na kuwekeza kabisa katika operesheni hii kubwa ya kijeshi sio ishara ya kuinyesha nguvu, bali kuonyesha udhaifu wa hali ya Assad. Kwamba ikiwa mtu ana nguvu, basi haupaswi kulituma jeshi lako kumsaidia mshirika wako".

Urusi ilikanusha kuwa iliishambulia hospitali yoyote, ikizitaja ripoti hizo kuwa ni “madai ambayo hayajathibitishwa”. Serikali ya Uturuki ambayo inasaidia magaidi nchini Syria inasema mashambulizi ya angani ya Urusi ya kumuunga mkono Assad ni ya kinyama na sasa inashinikiza mpango wa kuwapeleka wanajeshi wan chi kavu nchini Syria kwa usaidizi wa Marekani na mataifa ya Ghuba ili kuwasaidia magaidi ambao wanaelemewa na majeshi ya Syria.

Hapo jana, wizara ya ulinzi ya Marekani ilisema Saudi Arabia imeanza tena mashambulizi ya angani ya muungano unaoongozwa na Marekani dhidi ya vikundi tiifu vya serikali ya Syria vinavyoaopambana na magaidi wa Daesh nchini Syria. Uturuki pia imejikita katika vita vyake na wapigananji wa Kabila la wa Kikurdi kaskazini mwa Syria, ambao inaamini wana mafungamano na chama kilichopigwa mafuruku cha Wafanyakazi wa Kikurdi – PKK ambacho kimefanya uasi kwenye ardhi yake kwa miongo mingi. Urusi imesema mashambulizi hayo ya Uturuki ni ukiukaji mkubwa wa sheria.

Marekani na washirika wake wanajaribu kupanga mbinu za kuingia Syria kijeshi baada ya magaidi walokuwa wakiwatumia kushindwa kutimiza malengo, hali hii imetajwa kuwa ni ya hatari na inaweza kusabibisha moto usio weza kuzimika.

Mwisho wa habari/ 291