30 Machi 2016 - 18:02
Rais mpya wa Myanmar, Htin Kyaw aapishwa

Myanmar imeingia leo katika enzi mpya wakati vuguvugu la kidemokrasia la mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel Aung San Suu Kyi likichukua madaraka baada ya miaka 50 ya utawala wa kijeshi

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Myanmar imeingia leo katika enzi mpya wakati vuguvugu la kidemokrasia la mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel Aung San Suu Kyi likichukua madaraka baada ya miaka 50 ya utawala wa kijeshi. Mpambe wa karibu wa mtetezi huyo wa demokrasia, Htin Kyaw, ameapishwa leo kumrithi jenerali wa zamani Thein Sein ambaye aliongoza mageuzi yaliyoifanya Myanmar kubadilika kutoka taifa lililojitenga na kuwa hadithi ya matumaini ya kisiasa na kiuchumi. Chama cha Suu Kyi cha National League for Democracy - NLD kilishinda kwa kishindo uchaguzi wa Novemba huku kikipata asilimia 80 ya viti bungeni, hivyo kupewa jukumu la kuunda serikali. Rais mpya Htin Kyaw ameikaribisha enzi mpya ya serikali ya kiraia, akiahidi kuwa mwaminifu kwa watu na jamuhuri ya muungano wa Myanmar.

Mwisho wa habari/ 291