Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Ashton Carter amefanya ziara ambayo haikutangazwa mjini Baghdad, kwa mazungumzo na maafisa wa Iraq kuhusu vita dhidi ya kundi la kigaidi la Daesh, Ziara hiyo inafanyika baada ya wiki nzima ya mzozo wa kisiasa ambao ni pigo kwa Waziri Mkuu wa Iraq, Haider al-Abadi.
Carter amesema ni muhimu kumuunga mkono kiongozi huyo aliyeko kwenye mapambano na miongoni mwa maafisa atakaokutana nao ni al-Abadi na Waziri wa Ulinzi, Khaled al-Obeidi, kujadiliana namna ya kuongeza msaada wa kijeshi wa Marekani nchini Iraq kabla ya mapambano muhimu kwenye mji wa Mosul.
Marekani inaongoza muungano wa kimataifa ambao umefeli kunaendesha mashambulizi ya anga dhidi ya kundi la kigaidi la Daesh na pia inatoa mafunzo na msaada mwingine kwa vikosi vya waasi na magaidi nchini Syria ili kuiangusha serikali ya Bashar asad, jambo linalopingwa vikali na mataifa makubwa kama Iran, Urusi na China ambao wanapinga vitendo vya Marekani na washirika wake kusaidia magaidi badala ya kupambana na magaidi hao.
Mwisho wa habari/ 291