7 Mei 2016 - 14:12
Muda wa Usitishaji mapigano Syria  warefushwa kwa masaa 72

Usitishaji huu unahusu pande mbili ambazo ni upande wa jeshi la Serikali ya Syria unaoungwa mkono na Urusi na upande mwingine ni vikundi vya kigaidi vinavyoungwa mkono na Marekani na Saudia arabia.

Shirila la habari la ABNA linaripoti kuwa: Usitishaji wa mapigano wa muda katika eneo la mapigano nchini Syria katika mji wa Aleppo umerefushwa kwa masaa mengine 72 kuanzia leo Jumamosi tarehe 7 mwezi wa 5 mwaka 2016,wakati mapigano yakiendelea upande wa kusini.

Urefushaji wa kusitisha mapigano kwa ajili ya Aleppo unakuja wakati shutuma za kimataifa zinaongezeka kuhusiana na mashambulizi mabaya ya anga yaliyofanywa na magaidi wanaoungwa mkono na Marekani yaliyosababisha umwagikaji wa damu katika kambi kwa ajili ya watu waliokimbia makaazi yao kaskazini mwa Syria.

Wizara ya ulinzi ya Urusi imesema usitishaji huo tete wa mapigano umerefushwa "ili kuzuia hali kuwa mbaya zaidi" dakika chache kabla ya usitishaji wa awali wa saa 48 kwa ajili ya mji huo kumalizika.

"Hali ya utulivu katika jimbo la Latakia na mji wa Aleppo umerefushwa kutoka usiku wa manane Mei 7 kwa masaa 72," wizara ya ulinzi imesema katika taarifa.

Usitishaji huu unahusu pande mbili ambazo ni upande wa jeshi la Serikali ya Syria unaoungwa mkono na Urusi na upande mwingine ni vikundi vya kigaidi vinavyoungwa mkono na Marekani na Saudia arabia.

Marekani yathibitisha

Marekani  ambayo  inaunga mkono magaidi imekuwa ikifanya juhudi kuishawishi Urusi kuweka mbinyo kwa serikali kuzuia  mashambulizi dhidi ya magaidi wanaopewa msaada na Marekani na washirika wake na kufufua makubaliano ya kihistoria ya nchi nzima ya kusitisha mapigano yaliyofikiwa mwezi Februari  .

"Wakati tunakaribisha urefushaji huu , lengo letu ni kupata kufikia mahali ambako hatutakuwa tunahesabu masaa na kwamba kusitishwa kwa uhasama kunaheshimiwa nchi nzima Syria," amesema msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni ya Marekani John Kirby.

Jumuiya ya kimataifa ina matumaini kwamba kupungua kwa mapigano kunaweza kuimarisha mazungumzo yanayolegalega ya amani kumaliza miaka mitano ya vita ambavyo vimeuwa zaidi ya watu 72,000 na wengine milioni kadhaa kukimbia makaazi yao.

Utulivu umerejea katika mitaa ya Aleppo baada ya kusitisha mapigano kuanza usiku wa manane siku ya Alhamis, na kuwapa wakaazi unafuu kidogo kutoka wiki mbili za mapigano ambapo magaidi  wakiwemo wale wanaoungwa mkono na Marekani wamesababisha kiasi ya raia zaidi ya 280 kuuwawa.

Mapigano ya hapa na pale

Lakini kusini mwa mji huo, mapigano ya hapa na pale baina ya majeshi ya serikali na makundi ya kigaidi yanayoungwa mkono na Marekani pamoja na washirika wao yamewauwa zaidi ya magaidi  70, Magaidi wanaodhamini wa na Marekani kwasasa wapo katika hali ngumu kutokana na kuzingirwa na majeshi ya serikali.

Kundi la kigaidi la Al-Nusra na washirika wao ambao wanadhaminiwa na Marekani wametumia makubaliano hayo ya usitishaji wa vita kukiteka  kijiji cha Khan Tuman na vijiji vinavyozunguka eneo hilo chini ya masaa 24, baada ya majeshi yanayoiunga mkono serikali kuwafurusha kutoka eneo hilo mwezi Desemba.

Wanawake na watoto wanaripotiwa kuwa miongoni mwa wale waliouwawa katika mashambulizi ya Alhamis katika kambi karibu na mpaka na Uturuki, ambapo pia watu 50 wamejeruhiwa.

Mamun al-Kahatib , mkurugenzi wa shirika la habari linalounga mkono magaidi mjini Aleppo, ameshutumu kile alichosema kuwa ni "ndege za utawala" kwa kushambulia kambi hiyo katika kijiji cha Al-Kammouna siku ya Alhamis shutuma ziliungwa mkono na wadhamini wa magaidi lakini taarifa ya kuthibitika ikaja kufichua kuwa mashambulizi hayo yamefanywa na magaidi hao wanaoungwa mkono na Marekani na washirika wake.

Imekuwa ni ada kwa Marekani na washirika wake kuitupia lawaza serikali ya Syria katika matukio yakinyama yanayofanywa na magaidi wanaodhamini wa na Marekani na washirika wake.

Mwisho wa habari/ 291