Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: vyanzo vya Iraq vimetangaza kuwa: majeshi ya Iraq katika mwendelezo wake wa kuikomboa Fallujah wamefanikiwa kuikomboa miji mipya iliopo kusini mwa mashariki mwa Fallujah.
Majeshi hayo yamekomboa eneo la Buhairat na kaskazini mwa Rufeh katika sehemu ya Karmeh nchini humo.
Hatua ya tatu ya mashambulizi ya kuikomboa Fallujah nchini Iraq imeanza siku ya Alhamisi ya wiki iliopita.
Majeshi ya Iraq siku ziliopita yamefanikiwa kukomboa maeneno ya Abu Khamsini, Abu Khalid, Abu Aswi na Abu Saziy baina ya mji wa Amiriyah na Salam kusini mwa Fallujah na kukomboa maeneo hayo kutoka mikononi mwa magaidi wa Daesh.
Majeshi ya Iraq tuka tarehe 23 mwezi uliopita wakisaidiana na majeshi ya anga wanaendelea kufanya mashambulizi ya kuzikomoa sehemu tatu muhimu ambazo ni Dulabu, Zakhikhah na barabara ya kuunganisha mawasiliano baina ya Bagdadi na wilaya Hit iliopo katika mkoa wa Anbar.
Katka hali hiyo pia majeshi ya Iraq yamepambana na magaidi wa Daesh ya waliokuwa wamekusudia kuvamia mashariki mwa wilaya ya Haditha iliopo magharibi mwa mkoa wa Anbar na kuwaangamiza magaidi 16 wa kikundi cha Daesh.
Kadhalika magaidi wa Daesh walifanya mashambulizi katika sehemu ya “Jibalu Hamrain” iliopo mashariki mwa mkoa wa Salahu Dini, ambapo baada ya mashambulizi makali majeshi ya Iraq yaliwasambaratisha magaidi hao na kusababisha kuangamia magaidi 25 wa kikundi cha Daesh.
Kikundi cha kigaidi cha Daesh toka mwanzoni mwa mwaka 2015 waliyateka maeneo kadhaa ya nchi ya Iraq, ambapo majeshi ya Iraq kwa kipindi cha miezi kadhaa iliopita wamefanikiwa kuyakomboa maeneo kadhaa ya kaskazini mwa magaribi mwa nchi hiyo na kuwasambaratisha magaidi wa Daesh waliokuwa wameyateka maeneo
mwisho wa Habari/290