10 Mei 2016 - 16:00
Walioshambulia msafara wa maombolezo ya Imam Kadhim (a.s) wakamatwa

Kikundi kimoja cha kigaidi kilichokuwa na fungamano na kikundi cha kigaidi cha Daesh nchini Iraq kilifanya shambulizi kigaidi kwa msafara wa maombolezo ya Imam Kadhimayni (a.s) yaliofanyika mwezi 25 mwezi wa Rajab mwaka huu katika mji wa Kadhimain.

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: mtandao mmoja wa kikundi cha kigaidi ambacho kiko chini ya kikundi cha kigaidi cha Daesh ambao walifanya mashambulizi ya kigaidi kwa waumini waliokwenda kumzuru Imam Kadhim (a.s) wakamatwa na kusambaratishwa katika mjini wa Baghdad Iraq.
Waziri wa ulinzi nchini Iraq amesambaza habari kuhusu kikundi hicho nakusema: kikundi cha magaidi hao walitega mabomu kadhaa na walikuwa na vifaa kadhaa vya kuripua katika barabara inayokwenda haram ya Imam Kadhim (a.s) ambapo walijiandaa kufanya mashambulizi hayo.
Magaidi hao 5 baada ya kukamatwa walikiri kuwa lengo lao lilikuwa kutega mabomu katika magari watakayo watu wanaokwenda kumzuru Imam Kadhim (a.s) sehemu ya “Karadeh Dakhiliy” pia katika daraja la “Al Jadiriyah” mjini Baghdad.
Kadhalika majeshi ya Iraq yamekuta mabomu kadhaa yaliokuwa tayari kwaajili ya kufanya mashambulizi dhidi ya wageni wanaokwenda kumzuru Imam Kadhim (a.s) mjukuu wa Mtume Muhammad (a.s) katika mji wa Kadhimain nchini Iraq, hivyo wizara ya ulinzi ya nchi hiyo imewakabidhi magaidi hao kwa vyombo vya kisheria kwaajili ya hukumu.
Siku ya maombolezo ya kuuwawa kwa Imam Kadhim (a.s) nchini Iraq gari mbili ziliokuwa zimetegwa mabomu ziliripuka katika mji wa Baghdad na kusababisha vifo vya waombolezaji 20 pamoja na majeruhi.