13 Juni 2016 - 20:34
Mripuko wa bomu la gari wajeruhi tisa Uturuki

Bomu la kwenye gari limeripuka leo katika mkoa wa Tunceli ulio na Wakurdi wengi mashariki mwa Uturuki na kujeruhi watu tisa, ukiwa mripuko wa karibuni zaidi katika nchi hiyo inayoshuhudia vurugu.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Bomu la kwenye gari limeripuka leo katika mkoa wa Tunceli ulio na Wakurdi wengi mashariki mwa  Uturuki na kujeruhi watu tisa, ukiwa mripuko wa karibuni zaidi katika nchi hiyo inayoshuhudia vurugu. Kituo cha CNN Turk kimeripoti kuwa mripuko huo umetokea nje ya jengo la mahakama katika wilaya ya Ovacik. Mikoa ya mashariki na kusini-mashariki mwa Uturuki inakabiliwa na mapigano ya kila siku kati ya vikosi vya serikali na wapiganaji wa Kikurd, baada ya mapatano ya kusitisha mapigano na mazungumzo ya amani kuvunjika mwaka uliyopita. Serikali ya Uturuki imeondoa uwezekano wowote wa kurudi kwenye meza ya mazungumzo. Wakati huo huo, kundi lenye msimamo mkali lililojitenga na kundi kuu la Wakurd la PKK - linalojiita Kurdistan Freedom Falcons TAK, na ambalo lilidai kuhusika na shambulio la wiki iliyopita mjini Istanbul ambamo watu 11 waliuawa wakiwemo askari polisi sita, limesema alikuwa mripuaji wa kujitoa muhanga aliefanya shambulizi hilo.

Mwisho wa habari/ 291