1 Julai 2016 - 11:23
Mapigano kati ya Serikali na magaidi yashadidi Syria

. Mgogoro wa Syria unaochochewa na Marekani na washirika wake ambao umedumu kwa miaka mitano umesababisha vifo vya zaidi ya watu 280,000.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Watu wasiopungua 70 wameuwawa kufuatia mapigano kati ya majeshi ya serikali na makundi ya kigaidi yanyoungwa mkono na Marekani na washirika wake yaliodumu kwa masaa 24 huko Kaskazini mwa Syria.

Shirika la Uangalizi wa Haki za Binaadamu limesema wanajeshi 30 na wapiganaji magaidi wanaopewa silaha na Marekani zaidi ya 40  wameuwawa katika mapigano yaliotokea katika maeneo ya Al-Maleh, kaskazini mwa Aleppo tangu jioni ya Alhamisi. Wapiganaji wa kundi kigaidi la la Al-Nusra, linalotajwa kuwa tawi la al-Qaeda nchini Syria vilevile ni miongoni mwa waliuwawa.

Serikali ya Rais Bashar al Assad imekuwa katika jaribio la kutaka kulidhibiti eneo la Al-Maleh kwa zaidi ya miaka miwili sasa. Jeshi lake kwa miezi kadhaa limekuwa likijaribu kuuzingira mji wa Aleppo kwa kuzuia hudumua katika ya wilaya zinazodhibitwa na magaidi katika mji huo na karibu na Uturuki, ambayo inaunga mkono magaidi hao ikishirikiana na Marekani, Ulaya na baadhi ya nchi za kiarabu.

Jitihada za Urusi katika kutokomeza magaidi

Karibu wiki sasa majeshi ya utawala wa Syria, yakiungwa mkono na ndege za kivita za Urusi yamekuwa yakipambana vikali kuudhibiti mji wa Al-Maleh. Utawala wa Assad vilevile upo katika jitihada ya kuivuruga barabra muhimu ya Castello, inayotokea mpakani mwa Uturuki kuelekea vitongoji ambavyo vinakaliwa na magaidi wanaodhaminiwa na Marekani  vya Aleppo.

Tovuti inayoegemea upande wa utawala Al-Masdar imeripoti kuwa jeshi la Syria limejiondoa katika maeneo ya mashambani la Al-Maleh wakati wakikabiliana na mashambilizi makali yanayoongozwa na wapiganaji wa Kundi la kigaidi la Al-Nusra Front lenye mafungamano ya karibu na Marekani na Saudia arabia. Ripoti hiyo inasema magaidi waliyashambulia majeshi ya serikali kwa mabomu mawili ya kujitoa muhanga.

Shirika la uangalizi wa haki za binaadamu nchini humo limesema watoto wawili ni miongoni mwa waliuwawa kwa bomu katika eneo linalodhibitiwa na magaidi mjini Aleppo. Idadi kubwa ya maeneo ya jimbo la Aleppo yanadhibitiwa na magaidi wanaoungwa mkono na Marekani Al-Nusra Front na washirikia wao makundi mengine ya kigaidi yanayoungwa mkono na Marekani.

Lakini mkoa huo uliyokuwa mji mkuu wa kibiashara kabla ya vita, umegawanyika tangu Julai 2012. Kuna maeneo ya magaidi na mengine yanadhibitiwa na serikali.

Katika hatua nyingine shirika hilo la uangalizi vilevile jana liliripoti jana kuwa watu kumi na watatu, wakiwemo watoto wanne vilevile wameuwawa kwa makombora katika mkoa wa Ghouta Mashariki uliyoko karibu na Damascus. Mgogoro wa Syria unaochochewa na Marekani na washirika wake ambao umedumu kwa miaka mitano umesababisha vifo vya zaidi ya watu 280,000.

Mwisho wa habari/ 291