29 Julai 2016 - 07:42
Polisi waupekua msikiti Ujerumani

Polisi hapa Ujerumani imeupekua msikiti mmoja katika mji wa Hildesheim ambao umehusishwa na kundi la kigaidi la...

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Polisi hapa Ujerumani imeupekua msikiti mmoja katika mji wa Hildesheim ambao umehusishwa na kundi la kigaidi la Daesh linalojiita Dola la Kiislamu na kukusanya ushahidi wa kuunga mkono mipango ya kulipiga marufuku kundi hilo. Wizara ya Mambo ya Ndani ya jimbo la Lower Saxony imesema katika taarifa kuwa operesheni hiyo iliyowahusisha polisi 400 imefanyika jana usiku baada ya miezi kadhaa ya maandalizi. Maafisa wana ushahidi kuwa Waislamu msikitini humo wanapewa mafunzo yanayotoka Saudia Arabia ya itikadi kali na kuhimizwa kwenda kupigana katika maeneo ya vita, na kuwa baadhi ya waumini tayari wameondoka Ujerumani na kujiunga na mashirika ya kigaidi likiwemo kundi la kigaidi la Daesh linaloungwa mkono na mataifa makubwa ya kiarabu na washirika wako ili kuziangusha serikali  nchini Iraq na Syria lakini Urusi, Iran na China zimesimama kidete kupinga uovu huo.

Mwisho wa habari/ 291